Rais Joyce Banda amfukuza kazi Mkuu wa Polisi Malawi!

unajua kisa cha yeye kufukuzwa kazi na Mutharika? walitofautiana misimamo wa jinsi ya kuendesha nchi!

hii sasa ni riwaya yako.......................tofauti ni kuwa huyu mama aliona mutharika hamtaki kumrithi ndiyo maana akakimbia chama baada ya mutharika kupitisha jina la ndugu yake....sijui kaka yake.............kama angelimpitisha yeye angelibaki kusubiria kukamata dola huku akiunga mkono mambo yote ya bosi wake.........wanasiasa ni wanafiki sana.....it is all about their daily bread.......where........personal interests are permanent but mutual friendship is temporary.......
 
Hizo ndizo siasa za Africa za kukomoana

ni kweli shine......hapa tz mwaka 1995 Mkapa aliwafuta kazi makamishina wa polisi tulipomkemea tuliambiwa tumwache ajenge taifa............waathirika wake walienda mahakamani hadi Appeals Court na wakashinda kwa kishindo cha Tsunami na kulipwa kitita cha milioni 70 kila mmoja pamoja na haki zao nyinginezo............Mkapa aliendelea kupanga safu za wapambe wake akina Mahita ambao mwaka 2005 kila mmoja aliona hawafai..................life goes on, man na mkapa hajawahi hata kutuomba msamaha.

matatizo ya jamii siyo and ought not be a one man crusade.............
 
na kwa nini title yako inasomeka Mama Joyce Banda badala ya Rais Joyce Banda???

yeye kasema kuwa yeye ni mama kwanza halafu uraisi baadaye.............mama ni mpole na hana papara............na nimetumia hiyo lugha kumkejeli yeye mweyewe kwa kauli yake
 
sipingi yawezekana wana tuhuma za kujibu......ukiondoa mawaziri ambao sheria inamruhusu kuwaondoa hata bila ya sababu lakini mimi ninawatetea zaidi watumishi wa umma ambao kwa ajira zao walipaswa wapewe nafasi ya kujitetea...........kwenye chombo huria...................huyu mama ni adui wa utawala bora...................hawezi yeye kuwa ni hakimu kwenye kesi yake aliyojianzishia yeye mwenyewe.......................lol

Mkuu Rutashubanyuma.

Kwa kuzingatia nilicho-bold, naomba niseme kwamba Katiba nyingi za Afrika pamoja na sheria tunazotunga zina walakini sana na nyingi zinatungwa ili kumlinda Rais aliyepo madarakani na kumpa mwanya wa kufanya apendavyo bila kubanwa na sheria.

Hao watumishi wa umma wanapokuwa appointed na Rais hawana job security na imewekwa hivyo kwa makusudi kabisa ili mhusika "akiboronga" [hapa nina maanisha akifanya kinyume na matakwa ya Rais, hata kama alichofanya ni uamuzi sahihi kitaalam na kitaaluma] anaondolewa bila hata kutafuta sababu ya kumuondoa.

Ni sheria chache za presidential appointees ambazo zimeweka job security, kwa hapa Tanzania mfano ni Gavana na Manaibu wake wa Benki Kuu, Mkurugenzi wa TBC. Lakini pamoja na hayo muda wa miaka 4 au 5 ukiisha kama Rais "hajaridhishwa" na utendaji, anamtoa mhusika. Mfano mzuri ni namna Tido Mhando alivyotolewa TBC na kupelekea malalamiko kila kona, lakini hakuwa na mahali pa kwenda kushitaki, maana ni appointment ya miaka 4, muda ukiisha mteuzi anaweza ku-extend au akasitisha.

Kama hao watumishi wa umma wana job security na wanahisi wameonewa kwa kuondolewa bila kupewa nafasi ya kujitetea, mahakama zipo na sheria zipo. Hofu yangu ni kwamba hakuna vipengele vya sheria vinavyowalinda. Kwa hiyo Mama Banda anafanya hivyo kwa kuwa anajua kuwa walengwa hawawezi kwenda popote kudai haki zao kwa kuwa hakuna sheria inayolinda ajira/teuzi zao.

Mapungufu ya Katiba na Sheria yanatumiwa vizuri sana na marais wengi wa Afrika. Sheria nyingi zinazotungwa zinampa Rais madaraka makubwa ya kufanya apendavyo bila kuvunja sheria. Mfano mzuri ni hii Benki Kuu yetu, ipo siku Rais atakuja kuteua F6 or F4 leaver na hakuna atakayekuja kuhoji maana sheria inamruhusu. Sheria ya BOT imeweka vigezo vya elimu na uzoefu kwa Gavana tu, lakini Manaibu Gavana hakuna vigezo vya kuwateua. So, Rais anaweza kumpa ulaji yeyote yule hata kama hana sifa. Halafu Waziri wa Fedha alipobanwa Bungeni anasema unajua tukiweka na vigezo vya elimu na uzoefu kwenye nafasi za Naibu Gavana, tutakuwa tunambana sana Rais, tunatakiwa tumpe na yeye wigo mpana wa kuteua watu. Statement hiyo inaashiria kwamba teuzi sometimes ni kama zawadi na sio kwamba zinatakiwa kuangalia merit. Tuna wateule wengi tu ambao hawana sifa na ndio maana utashangaa tuna wakuu wa wilaya ambao hawajui hata Kiingereza na wanakiri hadharani.

Utawala Bora na Utawala wa Sheria una maana pale ambapo sheria hazina loopholes ambazo Rais anaweza kuzitumia kufanya madudu yake. Kwa nchi za Afrika Utawala Bora na Utawala wa Sheria bado ni msamiati, tuna safari ndefu sana. Tunatakiwa kuboresha Katiba pamoja na Sheria zilizopo, na hakuna Rais anapenda kufanya hayo maana akifanya hivyo anajua inajichimbia Kaburi yeye mwenyewe.
 
Huyu ni mama kweli wa shoka, amedhubutu. Hivi Tanzania ingekuwa hivi si pangekuwa kama Ulaya? one mistake out! Jk aliingia Pango la wanyang'anyi (Ikulu ) kimya hadi hivi leo -shame
 
Back
Top Bottom