Rais John Magufuli mjamaa aliyestahili kuongoza Tanzania baada ya Mwalimu Julius Nyerere

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
RAIS JOHN MAGUFULI,MJAMAA ALIYESTAHILI KUONGOZA TANZANIA BAADA YA MWALIMU JULIUS NYERERE.

Leo 14:15pm,15/12/2019.

Natafakari tu endapo Rais John Magufuli ndiye angekuwa aliyeachiwa kijiti cha Urais wa Tanzania mwaka 1985, yale maviwanda kama Kilitex, Sunguratex, TBL,Bora yaani ile Pugu road yote vilikuwa viwanda vya Serikali, hakika naamini leo hii tatizo la ajira lisingekuwa kubwa na pia naamini umasikini wa kipato cha mtu mmoja mmoja isingekuwa ajenda kwa sasa.

Nafahamu changamoto kubwa ya kiuchumi ambayo alianza nayo Rais Ali Hassan Mwinyi mwaka 1985 alipochukua kijiti cha Urais.

Awamu ya kwanza ya Rais Julius Nyerere viwanda vilijengwa na kuongozwa kwa mfumo wa kiujamaa ndio maana kulikuwa na viwanda vingi vya ushirika.

Tanzania ilipopata Uhuru mwaka 1961 Mwalimu Julius Nyerere aliongoza kwa mfumo wa kiujamaa ambao kwa mabeberu walipinga ilifikia hatua hadi kuhujumu bidhaa zitokazo ndani ya Tanzania.

Kulikuwa na jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo anguko lake ni moja ya hujuma iliyo fanywa na
wenzetu Kenya wakati wa Jomo Kenyatta na Uganda wakati wa Nduli Iddi Amini Dada.

Mifumo yao haikuwa ya kijamaa na waliuvaa ubepari kiasi kwamba ujamaa kwao ilikuwa kama kuchelewesha kuiba toka kwa Wananchi,

Ubepari wa Kenya na Uganda uliwafanya wawe watu wa kujipenda wenyewe na kuiga tabia ya wazungu ya kutawala nchi zenye tabia ya upole ,kwa maana upole ulitoka kwenye Ujamaa.

Nakumbuka ujio wa Fidel Castro nchini Tanzania na ujio wa Che Guevara ulipata kumshauri Mwalimu Nyerere juu ya Upole hasa katika Ujamaa ambao tumedhamiria kuenenda nao kama mfumo wa maisha yetu nchini Tanzania.

Hujuma nyingne ilikuwa ni anguko la azimio la Arusha,anguko la Azimio la Arusha lilisababishwa na kuinuka kwa ubepari ambao ulianza kuota mizizi miongoni mwa Wafanyabiashara.

Wafanyabiashara waliazimia kuanzisha Azimio la Zanzibar ikiwa ni ingizo la Wafanyabiashara katika nchi iliyokuwa ya Wafanyakazi na Wakulima,kuanzia hapo Wafanyabiashara walianza kushika hatamu na kuhodhi Mali ya Umma.

Naweka list ya viwanda vilivyopata kuwepo lakini vikahodhiwa na Wafanyabiashara wakubwa na kuviua, Tukumbuke ni hivyo Viwanda ndivyo ambavyo vilikuwa mkombozi wa ajira kwa Tanzania. Vingi viliajiri zaidi ya watu 1000. Mbali na viwanda hivi, kuna mashirika ya Umma ambayo sikuyaweka.Tunathamini juhudi kubwa ya kujenga viwanda katika awamu ya kwanza,hii ilikuwa enzi ya Mwalimu Julius Nyerere.

1. Polytex –Morogoro

2. Tanneries –Morogoro.

3. Leather industries –Morogoro.

4. Magunia –Morogoro.

5. Moro-Shoes –Morogoro.

6. Moproco –Morogoro.

7. Morogoro ceramic –Morogoro.

8. Mang’ula machine tools-Morogoro.

9. Mutex -Musoma,Mara.

10. Mwatex -Mwanza.

11. Nyanza glass –Mwanza.

12. Tanneries -Mwanza.

13. Urafiki –Dar es Salaam.

14. UFI –Dar es Salaam.

15. Sunguratexile –Dar es Salaam.

16. Mbagala glass –Dar es Salaam.

17. Tanganyika Parkers –Dar es Salaam.

18. Swala (Baiskeli) –Dar es Salaam.

19. National Panasonic –Dar es Salaam.

20. Bora –Dar es Salaam.

21. Sigara –Dar es Salaam.

22. Twiga chemical –Dar es Salaam.

23. Keko pharmacy –Dar es Salaam.

24. National Milling –Dar es Salaam.

25. Mbeya textile –Mbeya.

26. KIZAKU –Mbeya.

27. Magunia –Kilimanjaro.

28. Kilimanjaro Machine tools –Kilimanjaro.

29. Phillips –Arusha.

30. General Tyre –Arusha.

31 Scania – Kibaha Pwani.

32. Korosho- Kibaha Pwani.

33. Ginneries –Mwanza, Shinyanga, Morogoro.

34.Mbegu -Morogoro.

35.Canvas -Morogoro

36.Polyster-Morogoro.

Awamu ya tano,katika kipindi kifupi cha miaka 4 tumemshuhudia Rais Mjamaa,Mzalendo John Magufuli akirudisha Viwanda vilivyoporwa na kuhujumiwa,akirejesha na kuyafufua Mashirika ya Umma yaliyokufa,akijenga viwanda vipya ili kutengeneza ajira kwa mamilioni ya watu ambao hawana ajira,

Rais John Magufuli anasimamia kwa nguvu miradi mingi yenye thamani kubwa ya fedha na yote inatambaa kwa nguvu na speed kubwa.

Ni katika nchi hii hii tulipata kuaminishwa kuwa hakuna hela, hela zinapatikana nje ya nchi tu. Lakini leo hii katika nchi hii hii ya Tanzania Mheshimiwa Rais John Magufuli amesema hela zipo hapa hapa Tanzania na nje hatoki ng'oo.

Sasa tunashuhudia tukiendelea na ujenzi wa Reli ya Umeme,Bwawa kubwa la Umeme,Ununuzi wa ndege kubwa kumi na moja,Yote ni kwa fedha zetu na hatujakwenda kukopa kwa Mabeberu,miradi inakwenda vizuri. Ni lazima tujiulize hizi hela zilikuwa wapi?

Ni dhahiri katika kipindi cha miaka hii minne ambayo Rais John Magufuli amefanya Mapinduzi makubwa hata wazungu wasingeweza kwenda na hizi multiple and giant projects Kwa wakati mmoja.Narudia kusema Wazungu wasingeweza hata kidogo,kwa lugha ya beberu niwaambie Only a genius can do this.

-Rais John Magufuli abadili Upepo na kuleta Mapinduzi makubwa ya kiuchumi.

Kufaidika kiuchumi katika dunia hii ya leo kunahitaji kujitoa sadaka mbele ya uso wa Mabeberu,kuna changamoto nyingi lakini angalau awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli imefanikiwa kuifahamu vyema sana dunia na mahitaji yake.

Kero ni ule ukweli kwamba katika awamu karibu zote tatu kabla ya hii ya sasa kundi la wenye kutakiwa kuwa wazalendo ndio lilikuwa limejaa madalali wa kuiumiza na kuiuza nchi yao Tanzania nchi yao waliyozaliwa.

Vita ya kiuchumi sio vita ndogo, ukikaa pamoja na watu Wazalendo katika Awamu hii ya tano watakwambia ni kwa namna gani wanapambana na hao waliozoea kuiumiza nchi ambayo Baba na Mama zao wamezaliwa!.

Hizi pesa zinazoitwa gawio la kwenda hazina katika awamu zilizopita ndizo zilizokuwa zinaishia juu kwa juu zikistawisha maslahi ya wenye vyeo na marafiki zao na familia zao,ndio hao leo hii wanaongoza kwa kupiga kelele hela haipo.

Kila mwenye kujiona mzalendo na awe wa kwanza kuumizwa kila anapoona watu wanataka kutajirika kirahisi tu kwa kuiba Mali ya Umma huku Wananchi walio wengi wenye haki na nchi yao ya Tanzania wakibakia malofa.Tuunge mkono juhudi za Awamu ya tano,chini ya Rais John Magufuli.

-Rais John Magufuli ni Mwanafunzi mzuri wa Julius Nyerere na Niccolo Machiavelli.

Niccolo Machiavelli ambaye aliandika vitabu maarufu vya masuala ya Maslahi ya Taifa kama "The Prince" cha mwaka 1513 ambacho kilikuja kutafsiriwa kwa kiingereza mwaka 1532 na "The Discourses" cha mwaka 1517 ambacho kilikuja kutafsiriwa mwaka 1531 kama "The Discourses on livy".

Niccolo Machiavelli ni miongoni mwa waandishi waliokuwa wakihusudiwa sana na hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kudhihirisha hilo,katika moja ya mahojiano yake Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alisikika akisema;"You want me to tell you what's a book Iam reading now?....I'm reading Machiavelli ".

-Kwa nini nasema Rais John Magufuli ndiye aliyestahili kuchukua kijiti cha Rais Julius Nyerere.

•Kuweka mbele maslahi ya Taifa.

Niccolo Machiavelli (1513) alitumia neno "Raison d'etat" kwa kiingereza "Reason of the State" kuelezea kwa kina namna Rais wa Nchi anavyoweza kufanya lolote liwezekanalo ili kupigania na kulinda maslahi ya Taifa kwa kuwa rasilimali za Taifa ndiyo sababu ya uhai wa dola.

-Kulipa Kodi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Profesa Paramagamba Kabudi alisema akiwanukuu Waisrael na Wamarekani kuwa wao (Marekani na Israel) wanaamini katika mambo mawili;

1- Kuzifia Nchi zao.

2-Kulipa Kodi.

Tukumbuke pia Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alisisitiza Uzalendo na aliwahi kusema "Taifa lisilolipa kodi ni Taifa mfu".

-Rais John Magufuli ni Strategic Negotiator.

Kwa kuzingatia Maslahi ya Taifa Rais John Magufuli alituthibitishia kuwa yeye ni Strategic Negotiator kwa kutazama jinsi Serikali yake ilivyoingia kwenye majadiliano ya Madini ambayo tulikuwa tunaibiwa kila uchwao lakini hivi sasa tunagawana faida nusu kwa nusu.

Tuliona jinsi Serikali yake ilivyokataa mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo,mkataba wa kimangungo wa ujenzi wa Reli ya SGR uliokuwa ujengwe na Wachina kwa gharama mara mbili ya Ujenzi wa sasa,na namna alivyoshawishi bomba la Mafuta liweze kujengwa kutoka Hoima,Uganda mpaka Chongoleani,Tanga.

Nimalizie kwa kusema,Rais John Magufuli ndiye mbarikiwa mwenye kibali cha kuiongoza Tanzania machoni pa Mungu,Tuunge mkono juhudi zake kwa maslahi mapana ya Taifa la Tanzania,Tanzania isonge mbele ya kutopiga hatua kwa muda mrefu.

Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kumbariki Rais John Magufuli,Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kuibariki Tanzania.

Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
 
Hivi wewe unaamimini ktk historia ya mtu aliyekuwa mbunge, naibu waziri na hatimaye waziri kamili ktk kipindi ambacho madudu makubwa yalikuwa yakifanyika huku yeye akiwa bubu na hata mwenyewe kunufaika na madudu hayo? Mtu pekee naweza kuona uadilifu wake kutokana na matendo yake, mwenye kustahili kufuata nyayo za Mwl. Nyerere ni Edward Moringe Sokoine tu. Huyu ambaye unamsifu leo ngoja atoke madarakani na Magogoni ipate mkazi mwingine tuone kama hata utathubu kuandika uzi kama huu. Tatizo la Wabongo ni unafiki tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vijana fanyeni jitihada za kutafuta elimu sahihi, hasa elimu juu ya uchumi na maendeleo Tanzania. Mtajua mengi na kama mnaandika haya kwa kutumia akili zenu, basi mtakuwa wenye fikra tofauti kidogo na jumuishi.

Nawakumbusha tu baada ya Nyerere, kilichofuata ni "Economic Recovery Program" (ERP). Hicho ni kipindi ambacho, huku serikali ikipambana kurekebisha "mazalia" ya ujamaa mnaouna ni "right " policy kwa nchi yetu, kule bungeni kulikuwa na wa watu machachari akina Meja Abbas Ngayaga wakilia barabara ya kusini, akina Halfani Kihiyo wakililia barabara ya Segera-Tanga. Siwaambii barabara za kwenda sumbawanga, Tunduru nk zilikuwaje. Kama kila barabara muionayo leo imejengwa si zaidi ya miaka 20 iliyopita, je hali za barabara zetu zilikuwaje miaka ya 1980s? Ni Rais gani angewaza kujenga SGR?

Hebu nitajieni sekondari yoyote maarufu iliyojengwa nchi hii baada ya uhuru? Hebu jiulizeni, kama primary schools tuliweza kuwatumia walimu wa UPE, sekondari tulitumia walimu gani?

Tujifunze kuheshimu maamuzi yaliyofanywa katika kila awamu kwani yalifanywa kwa sababu zake ambazo kwa wakati huo yalikuwa ni ya kizalendo pia. 1980-1990 ni kipindi kigumu ever nchi ilichopitia. Hakuna mahitaji, hakuna miundombinu, sera za ujamaa zilishafeli, uzalishaji viwandani umekufa, ilibaki zamu ya "mabeberu" tu kuamua hatima ya nchi. Nyerere alianzisha majadiliano ya kurekebisha uchumi tangu baada ya vita vya idd amini bila mafanikio.

Everything was terrible and desperate, kwa maana ya terrible and desperate.

Nawatakia Noel njema.
 
Back
Top Bottom