Rais John Magufuli amemteua Dkt. Leonard Lutegama Maboko kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Leonard Lutegama Maboko kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS).

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu umeanza tarehe 07 Julai, 2016.

Kabla ya uteuzi huu Dkt. Leonard Lutegama Maboko alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya binadamu Mbeya (NIMR Mbeya).

Dkt. Leonard Lutegama Maboko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Fatma Mrisho ambaye mkataba wake umemalizika tangu tarehe 30 Juni, 2016.

Cm2J1QEWIAAiCTp.jpg:large
 
Rais Dr J. Magufuli amemteua Dr Leonard Maboko kuwa mkurugenzi mtendaji wa TACAIDS kuchukua nafasi ya FATUMA MRISHO mtu anayesemekana kuwa ndugu wa Kikwete kutokana na jina linaloonyesha ubini na rais huyo mstaafu
Mama huyo alizua mjadala siku za nyuma akihusishwa na Kikwete alipokuwa akiafanya kazi NIDA
 
Hizi teuzi zisizoisha zinaonyesha nchi hii ilivyokuwa imeoza ..... Au!!?

I am seriously confused!!
 
asante nchi inaendeshwa na DR na proffesa tu maana walizaraulika mbaya enzi za njomba!
 
Rais Dr J. Magufuli amemteua Dr Leonard Maboko kuwa mkurugenzi mtendaji wa TACAIDS kuchukua nafasi ya FATUMA MRISHO mtu anayetajwa kuwa ndugu wa Kikwete kutokana na jina linaloonyesha ubini na rais huyo mstaafu
Kama ulifikiri kwa hilo jina tu basi ni ndugu yake utakuwa umekosea sana maana kadri nijuavyo jakaya na mrisho yote ni majina yake na baba yake aliitwa halfan
 
Waache waendelee na maduka/ujasiriamali wao wanaoufahamu vizuri. Wachumi huita competitive advantage. Kwamba wanafanya vizuri zaidi kwenye ujasiriamali kuliko civil service. Tunafahamu pasipokuwa na shaka kuwa kosa lililofanywa na shemeji yao kuwaingiza kwenye civil service (TRA) liligharimu taifa kwa kiasi kikubwa.
 
Kila pahala changes du waume tuzidishe upendo kwa wake zetu maana ikijulikana una mgogoro au manyanyaso tu. Mkasi bila ganzi
 
Back
Top Bottom