Rais Jakaya Kikwete mstaafu, amekuwa Mwanademokrasia bora Tanzania.

Mkuu pilau waweza kuila kama ilivyo toka jikoni, lakini mlaji hupenda kuongezewa kachumbali, ndizi mbivu, maji ya baridi, juice nk. makala yako imekosa vionjo vya kufanya msomaji aburudike. jazia nyama mkuu tushawishike.
 
Mnasahau upesi sana kuwa wale masheikh wa Zanzibar waliwekwa mahabusu mpaka leo wako huko enzi za Kikwete; Ulimboka alifanyiwa unyama na watu wa Kikwete na mara zote waZanzibari wamenyang'anywa ushindi wa chaguzi zao huyo mnaemsifia ndio alikuwa Mtawala mkuu!! Hizo sifa zote zinatoka wapi?
 
Demekrasia ndiyo.... Upande wa pili Kikwete aliboronga kwenye uchumi. Jionee data

d418f6726069b81d2451ec853ee0aa01.jpg
 
Source yako ni ipi? Siamini World Bank eti ndio imeandika Mwinyi, Mkapa,Kikwete Magufuli kwenye hiyo graph.
Soma hii source rekodi kubwa kabisa ya GDP per capital ni ya mwaka 2015
Tanzania GDP per capita | 1988-2017 | Data | Chart | Calendar | Forecast
Hata hao WB wana rekodi zao tofauti

Tanzania | Data
Ndiyo WB hawajaandika hayo majina Mwinyi,Mkapa, Kikwete.... hayo majina yameandikwa kuonyesha msisitizo tu, na pia kuonyesha tofauti ya miaka waliyotawala maraisi.

Fahamu Kikwete alikuwa hayupo consistent kwenye uchumi. Anapanda anashuka, hapo inaonyesha uchumi ulikuwa haujengwi kwenye msingi imara.

Angalia data kuanzia 2005 anaingia hadi 2015 uone alivyokuwa anayumba. Mkapa ndiyo alionyesha consistency uchumi ulikuwa unakuwa bila kushuka kizembe.

2005

5d4996469a2efaf47184bc2fee4d8500.jpg


2015

fc86143754fdf7b31cd23f791af3886d.jpg
 
Back
Top Bottom