Rais Jacob Zuma atakiwa Kujiuzulu kwa Matumizi mabaya ya pesa za umma

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
7,869
16,913
Rais wa Afrika Kusini amekuwa katika kashfa ya matumizi mabaya ya pesa za umma kufanya matengenzo ya nyumba yake binafsi. wanasiasa mbali mbali wa ndani na nje ya nchi ya afrika kusini wamekuwa wakimtaka hivyo kwa muda mrefu. zuma alichofanya sana sana ni kuomba msamaha akisema ni mkanganyiko tu wa matumizi yaliyopitiliza ya pesa za umma.

dr poli mmoja ya wana harakati wa kiuchumi na siasa amesema suala la zuma ni uvunjifu wa katiba na alipaswa kujiuzulu. kelele hizi ambazo zimekuwa zikipigwa kla kona ya south afrika hazitoki tu kwa wapinzani, lakin hata ndani ya chama chake amekuwa akipigiwa kelele
zuma ni mmoja ya viongozi wa hovyo huku afrika ambaye anaongoza taifa kubwa sana katika afrika.

rais zuma amekubali kuzirudisha hizo pesa akisema kuwa hakuzitumia kwa nia mbaya. hata hivyo wapinzani wamesisitiza kuwa anapaswa ajiuzulu ama sivyo watapiga kura ya kutokuwa na imani naye. anc wamesisitiza kuwa wataendelea kumuunga mkono rais jacob zuma pamoja na makandokando yake katika uongozi.
 
Back
Top Bottom