Analogia Malenga
Platinum Member
- Feb 24, 2012
- 5,292
- 10,842
Emmanuel Macron aapa kuleta nafuu ya mfumuko wa bei nchini Ufaransa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron jana amefanya mkutano wa kwanza wa hadhara kabla ya kufanyika raundi ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini humo utakaofanyia Aprili 10.
Macron alizungumza na maelfu ya wafuasi wake huko Nanterre karibu na mji mkuu ukiwa ni mkutano pekee mkubwa alioufanya kabla ya uchaguzi. Macron aliwaahidi wafuasi wake kuimarisha haki ya kijamii na uwezo wa kununua bidhaa katikati ya mfumuko wa bei nchini Ufaransa.
Kulingana na Macron anayewania awamu ya pili, watumishi watapatiwa marupurupu yasiyokatwa kodi ya hadi Euro 6,000 na kuongeza kuwa serikali yake tayari imetenga karibu Euro bilioni 20 kwa ajili ya kudhibiti bei ya umeme na gesi kufuatia ongezeko la gharama za nishati.