Rais dkt. John pombe magufuli ashiriki misa ya krismasi katika kanisa la mtakatifu peter jijini dar

jme

JF-Expert Member
Aug 4, 2013
4,671
4,806
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na watanzania wote kuadhimisha Sikukuu ya Krismasi ambayo wakristo wote duniani huadhimisha siku ya kuzaliwa Yesu Kristo, zaidi ya miaka 2000 iliyopitaRais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wamesali ibada ya Krismasi katika misa takatifu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es salaamAkitoa salamu za Krismasi baada ya kukaribishwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam Mhadhama Kadinali Polycarp Pengo, Rais Magufuli amewatakia heri watanzania wote katika sikukuu hii ya Krismasi na kuwataka waishi kama ambayo Yesu Kristo aliishi, na kwa kutekeleza yote ambayo aliyafundisha.Ametoa wito kwa watanzania kuishi kwa amani, upendo na Mshikamano huku wakizingatia kufanya kazi, hasa wakati huu ambapo yeye mwenyewe anahamasisha uchapa kazi kupitia kauli mbiu ya "Hapa Kazi Tu"Rais Magufuli pia amewataka wakristo wote kuungana kuliombea taifa, kuwaombea viongozi na kuwaombea watanzania wote ili waweze kutimiza majukumu yanayowakabili."Ndugu waumini wenzangu, mimi ni yuleyule, nipo vilevile na nimekuja hapa kama Mkristo wa kawaida, muendelee kuliombea taifa hili na mtuombee pia sisi viongozi wake" Amesisitiza Rais Magufuli
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
25 Desemba, 2015

1wwvghqnb.jpg

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, Mkewe Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakishiriki Ibada ya Krismas katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam Desemba 25, 2015
e042b0ae-05f8-4a95-90e0-22b89f75990f.jpg

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akitoa salamu zake za heri ya Krismasi mara baada ya kumalizika Ibada ya Krismas misa ya kwanza katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam Desemba 25, 2015
fc2c89a7-62c3-42fd-8904-79e991f0c3a6.jpg
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam kasha akamkaribisha kusalimia wananchi baada ya kumalizika kwa Ibada ya Krismas misa ya kwanza katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam Desemba 25, 2015
 
Kila la heri kwake na serikali yake na heri zaidi kwa watanzania woote
 
Back
Top Bottom