Rais Bashir aomba Viza kusafiri Marekani

Rais Bashir aomba Viza kusafiri Marekani

Maswala

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2011
Posts
560
Reaction score
226
130216113248_omar_el_bechir_al_bashir_cairo_oci_0602_2013_144x81_afpgettyimages_nocredit.jpg

Rais wa Sudan Omar al-Bashir, ameomba hati ya usafiri kwenda nchini Marekani kwa mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa.
Mahakama ya kimataifa ICC, inamtaka Bashir kwa madai ya kuamuru mauaji ya halaiki na kuhusika na uhalifu wa kviita katika jimbo la Darfur.
Awali , vyombo vya habari vilisema kuwa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Ali Karti ataongoza wajumbe wa nchi hiyo kuhudhuria mkutano huo mjini New York.
Mara ya mwisho kwa Bashir kuzuru Marekani ilikuwa mwaka 2006.
Kibali cha kukamatwa kwa Bashir kilitolewa Mei mwaka 2009 na Julai mwaka 2010. Mahakama ya ICC imemshitaki kwa makosa kumi ya uhalifu wa kivita , uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya halaiki katika jimbo la Darfur.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Samantha Power, amethibitisha kuwa Marekani imepokea ombi la Viza kutoka kwa Rais Bashir.
Alitaja ombi hilo kama lisilofaa, la kuudhi na mzaha mkubwa kwa Marekani.
Msemamji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani, alisema kuwa wanalaani juhudi za Bashir kutaka kusafiri kwenda Marekani.
"Kabla ya kuja katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, alisema Bi Harf kuwa , "Rais Bashir mwanzo anapaswa kujikabidhi kwa Mahakama ya kimataifa ya Hague kujibu mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu anayokabiliwa nayo.’’
Hata hivyo Bi Harf hakusema ikiwa Marekani itamnyima Viza Bashir.
Gazeti la Sudan la Tribune linasema kuwa Marekani huwa na mipango maalum ya kisheria kuwapa viza maafisa wanaotaka kuhudhuria shughuli za UN ,mjini New York.
Kinachoweza kufanyika ni kuwa Bashir anaweza kukamatwa ikiwa atadhubutu kuingia nchini Marekani akielekea UN. Licha ya hayo, mtu yeyote licha ya uraia wake hawezi kuzuiwa kuingia katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa
Mwezi jana Saudi Arabia ilikataa kuipa ruhusa ndege iliyokuwa imembeba Bashir kuruka katika anga yake wakati Bashir alipokuwa anasafiri kwenda nchini Iran

BBC Swahili - Habari - Rais Bashir aomba Viza kusafiri Marekani

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
anaenda UN suala kwamba UN iko marekani ilo ni suala lingine.... ni kama alivyokwenda AU kule nigeria...
 
Back
Top Bottom