figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko kuwaa Mwenyekiti wa bodi ya Shirika Ia Viwango Tanzania(TBS).
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 23 Juni, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi inasema uteuzi huu umeanza tarehe 21 Juni, 2016.
Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Cuthbert Mhilu ambaye amemaliza muda wake.
Prof. Maboko ni Mhadhiri wa Jiolojia katika Chuo Kikuu cha Dares salaam (UDSM).
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Omari Ali Amir kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Omari Ali Amir alikuwaa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi inasema uteuzi wa Dkt. Omari Ali Amir umeanza tarehe 21 Juni, 2016.
Utaratibu wa kujaza nafasi ya Mkurugenzi Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa bahari kuu ni wa kubadilishana kila baada ya miaka mitatu kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, ambapo Mkurugenzi Mkuu akitoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi Naibu Mkurugenzi Mkuu hutoka upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kinyume chake.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam