Rais Awaruhusu Waendesha Bodaboda Pia Wasibughudhiwe!

Rais Awaruhusu Waendesha Bodaboda Pia Wasibughudhiwe!

Entareyehirungu

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2006
Posts
488
Reaction score
471
Wamachinga wanachekela wakati Ma-RC, DCs, Wakurugenzi wa Miji na Manispaa pamoja na Waziri wao wa TAMISEMI mikono iko shavuni na nyuso zimekunjamana huku wakiwa wameinamisha vichwa chini. Hii yote ni kutokana na agizo lililotolewa na Rais kutaka wamachinga wasibugudhiwe. Waachwe wafanye biashara wanavyotaka, pahala wanapotaka.

Wakati nikiwa ndotoni nikiandika hii makala, mahala fulani katikati ya ndoto nilihisii video na audio clips zilizovifikia vyombo vya habari pamoja na mitandao zimekatwa (zimechakachuliwa) na kuondolewa kipande kimoja kidogo ambacho Rais aliongeza kuwa wakitaka hata kutandaza bidhaa kwenye uwanja wa magogoni sasa ni “RUKSA”
CzIwkz9UkAEs7_4.jpg:large

Rais huyu anawependa kweli kweli wafanyabiashara ndogondogo zisizo rasmi a.k.a wamachinga! Nashawishika kuamini kuwa Rais anafahamu vema kuwa kutokuwa rasmi kwa wamachinga kunaaminisha pia Serikali kushindwa kupata kodi kutoka kwao. Na sitaki kuhisi kuwa Rais anajipinga katika jitihada zake za kutaka watu wafanye kazi na kulipa kodi.

Ila nataka niweke rehani kichwa changu kuwa wamachinga katika hili ni sawa na mchwa aliyeoteshwa mabawa, wakati yeye akishangilia kuwa sasa ataweza kuruka, hajuwi kuwa ndo hivyo anandaliwa mazishi na hatorudi kwenye kichuguu. Naweza kuandika kwa kujiamini kuwa wamachinga watakuja kuvunjiwa tena na kuondolewa siku za mbeleni. Wakati huo wataharibiwa mali na kupoteza mitaji mikubwa zaidi.
16299114_10155018313148069_7061084886832048265_n.jpg

Kutoka Gazeti la Mwananchi Alhamis, tarehe 2/02/2017​

Hizi operations za ondoa wamachinga, ondoa mama ntilie hazikuanza leo na wala lililofanyika halijaleta suluhisho la kudumu. Kilichofanyika ni kutoka kwa kauli na maamuzi ya kisiasa yenye kuleta afueni ya muda. Na yamkini kauli na maamuzi vimechochochewa na mambo mawili; mosi, ujumbe wa akina Lissu kwenye mitandao juu ya jinsi ya kuifaidi CCM na pili Mwanza kuwa ngome na langoni mwa njia ya mkulu kwenda nyumbani.

Wakati nikiwaza huu upendo na huruma ya Rais kwa wamachinga, nimeona “nimjaribu” Rais si kwa maono kama Lema bali kwa ombi maalum. Najua ombi langu si kubwa hata kidogo kwake na wala halitawabughudhi vijana wa Mangu. Nalo ni kumuomba rais awaruhusu waendesha bodaboda pia wasibughudhiwe.

Waendesha bodaboda wanawindwa kama nyumbu kwenye njia za kuingia mijini, wanaishi kama digidigi kwenye maeneo yao ya maegesho, wanabambikiwa kesi zisizo na miguu, wananyanganywa pikipiki na vijana wa “tiGo” pamoja na wale wenye sare nyeupe huku hatma ya pikipiki zao ikiwa ni kuozea kwenye viwanja vya vituo vya Mzee Mpinga. Kwa sasa njia rahisi ya kumuelekeza mgeni kituo cha polisi ni kumuambia aende mpaka ofisi yenye uwanja uliojaa pikipiki mpya, kuukuu na magofu. Tukumbuke hii ni mitaji ya vijana inayozikwa kwenye viwanja vya ofisi za serikali na bado tunalia na mitaji na vijana wasio na ajira! Itakuwa uamuzi wa busara kama Mkulu ataamuru bodaboda wasibughudhiwe.

Mwisho, mie nimeamua kujisemema kimoyomoyo asisikie mtu, kuendana na kauli mbiu ya nchi ya viwanda, vituo vingi vya polisi nchini vinazidi kujitosheleza ama kama viwanda vya spea za pikipiki au vyuma chakavu. Natania tu! Mayalla ni njaa kwa kisukuma

Updates:
Tarehe 17/02/2017-
Hali ya sintofahamu imeibuka jijin hapa baada ya machinga kuondoshwa kwa nguvu mjini hapa hasa Makoroboi eneo la msikiti

Maduka yamefungwa na huduma hakuna tena FFU wametenda kila kona ni noma
Naona mama mery tesha anajitaid kumuhalibia mabula ili makonda aje abebe jimbo kiulain
 
pia hata waliojenga mabondeni,walioingiza mifugo hifadhi za taifa na mapori ya taifa,waliovamia hifadhi za barabara
 
Ni kweli lazima kuwe na utaratibu katika mambo yote.
Katika mtazamo wangu ila naweza KUREKEBISHWA, Rais hakusema "Machinga WEKENI bidhaa zenu mlangoni mwa duka la mtu mwingine"

Nafikiri alikuwa anawasaidia ili watu WASIWANYANYASE bali sheria IFUATWE!
Haku- wa demean/Kuwadharau maofisa wake ikiwemo Mawaziri.Ila ilikuwa ni kutoa MWELEKEO! Mfano mzuri,

BODABODA IMEAJILI watu WENGI sana. Na KINACHOHITAJIKA ni UTARATIBU. Na ninaamini kwa MAWAZO yangu rais HATAMKASIRIKIA afisa yeyote ATAKAYEPANGA utaratibu muafaka MZURI katika changamoto kama hizo!
Lakini niko WAZI kurekebishwa kama nina mkosa!!
 
Ni kweli lazima kuwe na utaratibu katika mambo yote.
Katika mtazamo wangu ila naweza KUREKEBISHWA, Rais hakusema "Machinga WEKENI bidhaa zenu mlangoni mwa duka la mtu mwingine"

Nafikiri alikuwa anawasaidia ili watu WASIWANYANYASE bali sheria IFUATWE!
Haku- wa demean/Kuwadharau maofisa wake ikiwemo Mawaziri.Ila ilikuwa ni kutoa MWELEKEO! Mfano mzuri,

BODABODA IMEAJILI watu WENGI sana. Na KINACHOHITAJIKA ni UTARATIBU. Na ninaamini kwa MAWAZO yangu rais HATAMKASIRIKIA afisa yeyote ATAKAYEPANGA utaratibu muafaka MZURI katika changamoto kama hizo!
Lakini niko WAZI kurekebishwa kama nina mkosa!!
ni kweli ndugu tatizo uwelewa.
raisi alichokiona ni kuwa madc na rc, walikuwa bado hawajaandaa mazingira mazuri ya kuwapeleka wamchinga. amewaruhusu waendeleee hadi apo mazingira yatakapo andaliwa ndo wapelekwe.
 
Jana Rais Magufuli ameagiza Wamachinga wasibugudhiwe wanapofanya biashara zao.Tunaomba Na Waendesha Bodaboda nao waruhusiwe kuingia Mjini kufanya biashara.Marufuku hiyo ilizuiliwa hapo awali.
 
Back
Top Bottom