Rais ataka wakunga wa jadi wathaminiwe

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Rais Jakaya Kikwete ameitaka jamii kuwathamini na kuwasaidia Wakunga wa jadi kwa kuwa wanatoa mchango mkubwa katika kuwasaidia wanawake wakati wa kujifungua hasa vijijini.
Alitoa agizo hilo juzi usiku wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na hospitali ya CCBRT kwa ajili ya kuwashukuru wahisani mbalimbali walioipatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wazazi inayotarajia kujengwa jijini Dar es Salaam.
Hospitali hiyo itakuwa na hadhi zaidi ya zile za mikoa na itajengwa eneo ilipo CCBRT ambapo baada ya kukamilika itakuwa na uwezo wa kuwa na vitanda 200.
Akizungumza na wahisani hao, Rais Kikwete alisema Wakunga wana mchango mkubwa ikiwemo kuwazalisha akina mama hasa vijijini hivyo wanastahili kuthaminiwa.
Alisema asilimia 53 ya wanawake vijijini wanasaidiwa na Wakunga na idadi iliyobaki ndiyo wanaojifungulia katika vituo vya afya na hospitali za serikali.
"Mimi mwenyewe mama yangu alisaidiwa na wakunga aliponizaa na hakupata matatizo yoyote," alisema.
Aidha, aliwapongeza wahisani mbalimbali waliochangia fedha ili kufanikisha ujenzi huo na kuwataka wasichoke kufanya hivyo kila wanapoombwa.
Kwa upande wake, Rais wa Bodi ya Wakurugenzi katika hospitali hiyo, Dk. Willibrod Slaa alisema wahisani hao wamewasaidia Dola za Marekani 350,000.
Alisema wanahitaji Euro milioni 18 ili kukamilisha ujenzi wa hospitali hiyo na kwamba ili kupata fedha zaidi wamefungua matawi ya kuchangia katika nchi mbalimbali.
Kadhalika, allisema vifaa vya hospitali hiyo vitagharimu zaidi ya Dola za Marekani milioni 38.
Aliipongeza serikali kwa kuwasaidia ardhi kwa ajili ya kujenga hospitali hiyo hatua ambayo alisema iliwasaidia kupiga hatua.
Wahisani hao walipewa vyeti vya shukrani pamoja na kushikana mikono na Rais Kiwete.



CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Back
Top Bottom