Rais aionya Israel isithubutu kuichokoza Iran hata kidogo

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,890
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema uwezo wa majeshi ya Iran ni uwezo wa kumzuia adui na kuongeza kuwa, uchokozi hata mdogo zaidi wa maadui kama vile utawala wa Kizayuni wa Israel hautafumbiwa macho na vikosi vya ulinzi vya Iran.

Rais Ebrahim Raisi ameyasema hayo leo mjini Tehran alipohutubu kwa mnasaba wa Siku ya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Akihutubu katika gwaride hilo ambalo limeandaliwa katika Haram ya Imam Khomeini MA kusini mwa Tehran, Rais Raisi amesema, Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yana uwezo mkubwa sana. Amesema msingi wa uwezo huo ni wanajeshi wenye ikhlasi ambao wako tayari kuingia katika medani na kupambana na kila aina ya adui.

Rais ameuonya vikali utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kusema: " Utawala wa Kizayuni unafahamu kwamba harakati yake ndogo zaidi inafuatiliwa kwa karibu na majeshi yetu. Wakifanya kosa lolote, majeshi yetu yatafika katika kitovu cha utawala wa Kizayuni ambapo uwezo wa majeshi yetu hautawaacha katika utulivu."

Ameendelea kusema kuwa Jeshi la Iran limebadilisha vikwazo kuwa fursa katika sekta ya viwanda vya kijeshi na kufanikiwa kupata uwezo mkubwa.

Hali kadhalika amesema leo Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni jeshi ambalo lina zana za kutosha na liko tayari kuilinda nchi na mfumo wa Kiislamu. Ameongeza kuwa, kuwa tayari kivita Jeshi la Iran ni ujumbe wa matumaini kwa marafiki wa Mapinduzi ya Kiislamu nao maadui wafahamu kuwa uwezo wa majeshi ya Iran ni wa kujihami.

Rais amesema ujumbe wa uwezo wa majeshi ya Iran ni ujumbe wa nguvu kwa wote waliodhoofishwa, wanaodhulumiwa na wanaokandamizwa kwamba vikosi vya jeshi la Iran ndio nukta yao ya matumaini.
 
BigUp Iran lakini nasikitika sana Iran inashindwa kutusaidia hawa mazayuni ambao wanaitesa kunyanyasa waislamu Pakistan, Wazayun wamevamia Baitul Makdis na kujeruhi waislamu kadhaa na kuwaweka ndani ni muda sasa Iran kuunganisha dola ya Kiislamu na Pakistan
 
Nawapongeza sana Irani na North Korea kwa kukataa ujinga wa malekani wa kutaka yeye pekee na marafiki zake ndio wenye ruksa za kutengeneza na kumiliki siraha nzito na za kisasa.

Kwa kukataa ujinga huo wamejiweka safe zone kwa nguvu na taabu nyingi za vikwazo vya kiuchumi.
 
Back
Top Bottom