SONGOKA
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 1,841
- 1,843
Raisi unayeongoza nchi ambayo mapato ya ndani huchangia asilimia 57.8 (2015/2016) pekee ya bajeti, Wahisani wanapoanza kujitoa katika kuchangia bajeti sin tu ni janga la kitaifa bali huleta taharuki kwa wananchi na nchi nzima kwa ujumla, na kwa akili ya kawaida inakupasa kuwa ofisini muda huu.
Wananchi wamepaniki na wanahitaji kujua yafuatayo
Mheshimiwa, tulitegemea baada ya matukio haya ya kukimbiwa na wahisani, ungekuwa ofisini kwako ukizungukwa na wachumi wa hii nchi na wataalamu, ukijipanga na mwisho kuja kwetu sisi waajili wako na kutupa mipango yenye ufafanuzi wa hayo hapo juu.
Lakini kwa kuwa washauri wako wanaogopa kukwambia hili, naomba kukufikishia ujumbe na kukuomba urudi ofisini na uje kutupa ufafanuzi ili kuondoa hii taharuki
Wananchi wamepaniki na wanahitaji kujua yafuatayo
- Je hizo pesa ambazo tumezikosa tunazifidia vipi na kwa utaratibu gani??
- kujitoa kwa wahisani 10 wa ulaya kumeathiri vipi bajeti ya 2016/2017 ambayo maandalizi yake yanaendelea??
- Je kukosekana kwa hizi fedha kutaathiri vipi maisha ya mtanzania wa kawaida, hasa katika huduma za jamii na tozo za kodi??
- Je kutolewa katika mpango wa MCC na pia kujitoa kwa wahisani 10 wa ulaya kutaathiri vipi biashara kati ya Tanzania na hizo nchi?? na jumuia ya wafanya biashara ijipange vipi??
- Wote tunajua utalii unachangia GDP 17% na unaongoza kwa kuchangia foreign earnings (25%). na watalii asilimia 80% hutoka USA na UK, Je kwa hizi nchi kuitaja zanzibar kama undemocratic country itaathiri vipi idadi ya watalii kutoka nchi hizo??
- Je ofisi yako kwa kushirikiana na wizara ya fedha na mipango walikuwa na contingency plan??kama hawakuwa nayo, watuletee a fresh strategy inayoonyesha ni namna gani tutaweza vuka hiki kizingiti??
- kwa kuwa suala la Zanzibar limetuletea sisi innocent Tanganyikan adhabu hii, Je Zanzibar wanatu compensate vipi sisi watanganyika??
- waziri wako wa mambo ya nje alisema wametushika pabaya katika swala la umeme vijijini, je hii inamaanisha miradi ya REA ndo imesimama??
- kwa kuwa Uingeleza ndo nchi inaongoza kwa uwekezaji humu nchini, ikifuatiwa na USA, na ndo hawa umeanza kukosana nao katika misingi ya dermokrasia. Je hii italeta athari gani katika uwekezaji huu??
- mwisho, kwa kuwa ulituambia swala la uchaguzi wa Zanzibar halikuusu na halituusu sisi watanganyika, na wewe kama rais huwezi kuliingilia. Je sasa ambapo madhara yake yametuhusu ni nini kauli yako??