Rais afanya mazungumzo na waziri wa maendeleo Dernmark na rais wa awamu ya tatu leo Ikulu

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 19 Januari, 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi wa Denmark hapa nchini Mhe. Einar Hebogard, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.

Mhe. Martin Bille Herman amesema katika mazungumzo hayo wamejadili kuhusu uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Denmark na pia wamekubaliana kuuimarisha zaidi hususani katika masuala ya maendeleo ya kiuchumi.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Rais Mkapa amesema lengo la kukutana na Mhe. Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kumpa taarifa juu ya kazi anayoendelea kuifanya ya kuwa mwezeshaji wa mazungumzo ya mgogoro wa kisiasa nchini Burundi.
Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
1484834229881.jpg
 
View attachment 461679
Ningeona video ya hayo mazungumzo ningefurahi sana
 
Jpm mtu ambaye huwa anamuogopa na kumsikiliza ni Huyu mzee wa Malofa angalau wanapatana
 
Back
Top Bottom