Maoni yangu kwa wanahabari wote, waliotajwa hapa na wasiotajwa wote wabadilike. Na sisi wana JF pia tubadilike, tusitake kulazimisha watu kuwa wanachama wa vyama vyetu. Kuwa CCm au CDM ni uhuru wa mtu, lakini kwa wote hawa ku support mabadiliko ni lazima, WABADILIKE SASA HIVI! Hatuhitaji kujua chama cha mtu, tunahitaji wanaharakati wa MABADILIKO hata kama wako CCM. Kimsingi tunahitaji mashushushu wa mabadiliko walioko CCM, hawa ndio watatusaidia kubaini na kudhibiti wizi wa kura na kukamata masanduku ya kura kwenye mipaka ya Tunduma n.k.
By the way, kila mtu anapenda kulinda kibarua chake, wanahabari walioenda shule washike nidhamu ya kazi zao. Kuna wengine kama wa kule Clouds hawajaenda shule, naongea na wale walioenda shule.