Raila Odinga wa Tanzania apatikana

Raila Odinga wa Tanzania apatikana

kmasanja

Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
6
Reaction score
5
Siasa za Afrika mashariki hususani Kenya na Tanzania ni tofauti sana na nchi nyingine afrika, mwaka 2002, aliyeitwa profesa wa siasa za Kenya Mzee Daniel Arap Moi alishuhudia anguko kubwa la KANU baada ya kukaidi aliyoelezwa na watu wake kuwa mgombea anayemtaka ambaye sasa ni rais wa kenya Uhuru kenyata asingeweza kushinda maana by that time hauziki.

Team iliyoongozwa na Raila odinga iliweza kufanya kile ambacho wengi hawakuelewa maana yake , kwa nini waliamaua kumpa urais Mwai kibaki mshirika wa karibu wa MOI? swala halikuwa kujenga Kenya mpya swala lilikuwa kuhakikisha kwanza KANU inakufa mengine baadaye, Mwaka 1992 Kenya ilishuhudia uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi ambapo KANU iliviaangusha vibaya vyama vya upinzani, Raila Odinga kwa kugundua hilo baadaye kabisa aliaamua kuunganisha chama chake na KANU na kikaundwa chama kilichojulikana kama Newa KANU na Raila akiwa Executive secretary wa New KANU ambapo alisaidia sana kuisamabaratisha KANU.

Hapa Tanzania baada ya miaka 20+ ya vyama vingi dalili za kuitoa ccm madarakani, sasa naona Dalili za CCM kufa zimefika, RAILA wa Tanzania atakuwa ni ndugu Edward Ngoyai Lowasa, niko tofauti sana na wanaobeza lowasa kujiunga upinzani, miaka hii mitano tusitafute Rais wa maendeleo, kama tumevumilia miaka 50 bila maendeleo na maisha magumu kwa nini tusivumilie hii miaka mitano?

Rais ajaye kutoka upinzani awe ni special kwa kuvunja CCM na mabaki yake mpaka alama za CCM zisiwepo nchini, baada ya hapo, tuchague basi rais wa maendeleo.

Nahitimisha kwa kusema karibu Edward Lowasa CHADEMA ututoleee huu uchafu unaoitwa CCM Tanzania
.
 
Karibu luwasa cdm tuizike ccm milele

lowassa pekee hana uwezo wa kuitoa ccm madalakani kwani kura ya lowassa ni moja wenye uwezo wa kuitoa ccm ni watanzania tena wale waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la uchaguzi na wawe tayali kupiga kura na kulinda kura zao
 
Nimeipenda sana hii. Big up mleta mada kwa analysis yako nzuri!
 
CCM ife kwanza,mambo mengine baadae ase!!Ila tusisahau CCM ni "chama dola" hivyo nguvu kubwa inahitajika,yaani hadi goli la mkono lisisaidie
 
Nimeshawishika kuandika kwenye uzi wako kwa sababu moja kubwa kwamba ili yaitwe mabadiliko lazima ukubali kuvunja kilichopo kwanza na ndipo upate mabadiliko,sasa katika mazingira yaliyopo ili tuweze kupata mabadiliko vema tuondokane na zimwi ccm,na ukweli uliodhahiri ni kuwa mtu wa kumburuza Dr.J.P.Magufuli ni Mh.Lowasa na chama cha Mapinduzi kitafia hapo hapo,then tutakuwa na wakati wa kujenga nchi yetu tutakavyo kwa kuwa watakao ingia pia watakuwa na woga wa kuondolewa,ushawishi pekee ni kuleta maendeleo kwa wananchi.
Lowasa ni mtu muhimu kwasasa katika Siasa za Mageuzi katika upinzani kuliko wakati mwingine wowote.
Na viongozi wetu wa upinzani wanappreach mabadiliko na wao wawe radhi kubadilika na si kubaki na fikra zile zile za umimi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom