Raila Odinga aongoza mkutano wa hadhara katikati ya Jiji la Nairobi kuandaa wafuasi kwa maandamano ya Jumatano

Kenyan

JF-Expert Member
Jun 7, 2012
414
313
Imekuwa ni siku iliyowashangaza wengi baada ya Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga kutumia daladala kuelekea mjini na baada hapo kula chakula vibandani kwa mama ntilie.

Baadae msafara wake uliwasili mjini ambapo amezungumza kwa uchungu mkubwa kati kati ya Jiji akisema Rais Ruto anaamtaka kumwinda.

'Huyu Ruto Kila siku ananiwinda lakini ajue yupo' amesema Odinga.

Upinzani umepanga kufanya maandamano mengine siku ya Jumatano huku wengi wakihisi huenda yakawa ni makali zaidi ikizingatiwa kuwa Viongozi wengi wanaomuunga mkono Rais Ruto wameomba akamatwe sasa.

Ikumbukwe maandamano yaliyofanyika Ijumaa iliyopita yalipelekea vifo vya watu 6 huku wengine wakiuguza majeraha.
 
Siasa za kenya kumkamata odinga itawawia ugumu kidogo asee.Japo serikal ina uwezo huo
 
Back
Top Bottom