Raia wa Libya wajuta kuuwawa kwa Ghadhafi

Raia wa Libya wajuta kuuwawa kwa Ghadhafi

MOTOCHINI

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
29,097
Reaction score
35,476
RAIA wa Libya sasa wameanza kujutia kifo cha aliyekuwa kiongozi wao Muammar Gaddafi aliyeuawa miaka mitano iliyopita huku wakisema kuwa hali ya maisha imekuwa ngumu nchini humo.

Wakazi wanaoishi katika mji wa Tripoli wanasema kuwa bei ya mafuta, vyakula na huduma nyinginezo imeongezeka maradufu tangu kuuawa kwa Gaddafi.

Kuongezeka kwa gharama ya maisha kumesababishwa na kuchipuza kwa makundi mawili hasimu yanayopigania kudhibiti taifa hilo lenye utajiri wa mafuta.
“Maisha yangu yalikuwa bora chini ya utawala wa serikali ya Gaddafi.

Siku hizi tunalizimika kupanga foleni kwa zaidi ya saa 10 tukisihi wahudumu wa benki kutupatia fedha zetu,” akasema Fayza al-Naas, 42, ambaye ni daktari.
“Fedha zimetoweka na bei ya bidhaa ni maradufu,” akaongezea.
Juhudi za serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa (UN) kujaribu kudhibiti nchi hiyo zinaonekana kugonga mwamba baada ya bunge la serikali ya waasi kukataa kujisalimisha kwake
Ijumaa, serikali inayoungwa mkono na UN ilipatwa na pigo baada ya serikali ya waasi kunyakua sehemu ya mji wa Tripoli na kuweka afisi zake.

Wapiganaji wa kundi la Islamic State (ISIS) mnamo Juni 2015, waliteka mji wa Sirte ambapo Gaddafi alizaliwa.

Majeshi ya serikali ya muungano inayoungwa na UN kwa miezi mitano sasa yamekuwa yakipigana na waasi katika juhudi za kutaka kudhibiti mji wa Sirte.

Majeshi ya serikali ya muungano yanatekeleza mashambulio ya angani kwa ushirikiano na wanajeshi wa Marekani.

'Mwokozi wa Libya'

Bunge la waasi sasa linaunga mkono Khalifa Haftar ambaye amejitaja kuwa 'mwokozi wa Libya’.
Kulingana na mtaalamu wa masuala ya Libya Mattia Toaldo, nchi hiyo huenda ikaendelea kuwa na msukosuko kwa muda mrefu kwani matumaini ya serikali pinzani kuungana ni hafifu.

Vurugu zinazoshuhudiwa nchini Libya zimetoa mwanya kwa biashara ya ulanguzi wa watu kushamiri huku mamia ya wahamiaji wakikimbilia katika mataifa ya Ulaya kwa kuhatarisha maisha yao baharini.

Machafuko nchini Libya yamesambaa hadi katika taifa jirani la Tunisia ambalo limekuwa likishuhudia mashambulizi ya mara kwa mara.

Baadhi ya raia wa Libya, hata hivyo, wanasema kuwa machafuko yanayoendelea kushuhudiwa nchini humo yalisababishwa na utawala wa kidikteta wa Gaddafi.

“Shida zinazokumba Libya zilitokana na utawala wa kidikteta wa miaka 42 wa Gaddafi,” akasema Abderrahman Abdelaal, 32.

Gaddafi aliuawa akiwa na umri wa miaka 69 na majeshi ya muungano wa NATO mnamo oktoba 2011 mjini Sirte baada ya makabiliano ya muda wiki kadhaa.
 
Huu sio wakati wa kulaumiana kwa sababu hata angekuwepo gadafi labda hali ingekuwa mbaya zaidi hapo.
Cha msingi walibya inabidi wasiangalie walipo jikwaa ila waangalie walipo angukukia.
 
Well lakini naye aliua wengi sana na watu mnasahau NATO walimwambia acha kuua wananchi wako lakini hakusikia na yule mwanaye (jina???) ndio alikuwa akiongoza vikosi vya kijeshi kuwafyeka Libyans waliokuwa kwenye maandamano ya Arab spring,na Libya ina utajiri wa kufa mtu kiongozi yeyote kwa jitihada ndogo tuu angeweza kuwapa wananchi wote maisha bora na inawezekana Libyans wangekuwa na maisha mazuri zaidi bila hata Gadaffi, alipoteza more than 20 yrs to defend terrorist wateka ndege nchi yote ikawekewa vikwazo kwa ajiri ya ubabe wa kibwege tuu something he could avoid , oil price imeanguka sana na nchi zote zinazotegemea mafuta zinaanguka vibaya sana sio Libya tuu,angalia Venezuela,Nigeria even Russia wote in recession
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom