hamis77
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 18,465
- 27,064
Raia wa Gaza sasa akili zimerudi
Waikataa Hamas lakini Hamas wamewamininia risasi waandamanaji. Trump alisema Hamas itaenda kuishi kuzimu, huenda maneno yake yanaenda kutimia. Viongozi wa Hamas hawana pa kujificha tena, maana kila sehemu wanakoenda wanauawa. Israeli juzi ililipua hospitali ya Uturuki iliyopo Gaza na kuangamiza rundo la wapiganaji wa Hamas waliojificha humo.
Uturuki imeilaumu Israeli na Israeli pia imeilaumu Uturuki kwa kuwasaidia Hamas kwa siri. Toka mwaka jana Uturuki na Israeli hazina uhusiano mzuri. Huenda huko baadae Edrojen akaondolewa madarakani. Kuhusiana na maandamano ya Gaza, BBC wameripoti hivi; 👇
"Waandamanaji walikusanyika karibu na kambi ya watu waliokimbia makazi yao huko Beit Lahia, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, na kisha kuandamana kupitia barabara zilizozingirwa na vifusi vya majengo na nyumba zilizoharibiwa wakati wa vita, karibu na Hospitali ya Indonesia, ambapo waliimba nyimbo ukiwemo na kutoa kauli ikiwemo "Hamas out, out," kulingana na video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Wanachama wa Hamas waliojifunika nyuso zao, baadhi wakiwa na silaha na wengine wakiwa wamebeba marungu, waliwatawanya waandamanaji kwa nguvu na kuwashambulia baadhi yao."
👆Hivyo kwa taarifa hii ni dhahiri Hamas itaenda kuanguka na Gaza itaewekwa chini ya utawala wa Wayahudi kama ilivyo kwa maeneo mengine wanayoishi Wapalestina.
Greater Israeli inaenda kuundwa kwa uhakika machoni petu. Nitakuja kuelezea siri iliyo nyuma ya greater Israeli.