Raia nane wa China washikiliwa na wizara ya kazi na ajira kwa kufanya kazi nchini bila vibali

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Raia nane wa kichina wameshikiliwa na wizara ya kazi,ajira,vijana na watu wenye ulemavu katika ziara ya kushtukiza iliyofanywa na naibu waziri wa wizara hiyo Mh. Anthony Mavunde katika viwanda viwili hapa jijini Dar es Salaam na kubaini hawana vibali halali vya kufanya kazi hapa nchini.

Zoezi hilo la kushtukiza limefanywa na naibu waziri wa kazi,ajira,vijana na watu wenye ulemavu Mh Athony Mavunde akiongozana na maafisa kutoka wizarani pamoja maafisa kutoka ofisi za wakala wa afya na usalama mahala pa kazi-osha katika viwanda viwili mali ya raia wa China,ambapo katika kiwanda cha Wen xing kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam,kabla ya Mh naibu waziri kutoa maagizo na kuwashikiliwa wachina wanne upande wa kiwanda hicho haya yakaibuka.

Katika kiwanda cha Shuntao kilichopo Mikocheni raia wanne walishiliwa kwa kuwa na vibali visivyo halali.

Chanzo: ITV
 
Mie naona usanii tu yaani inamaana haiwezekani kufanya ukaguzi bila vyombo vya habari na waziri ??
viwanda ndiyo hivyo sasa nyie mnaleta mambo ya kukomoana, Ushauri wangu kwa wizara husika, wekeni utaratibu usiokuwa na urasimu natumaini hao wawekezaji watazingatia na kuufuata. sasa mnachofanya "AMBUSH" kwa wachunguzi wa mambo ni mazingira ya RUSHWA,
 
Back
Top Bottom