Ernesto Che
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,114
- 293
Mawazo ni mazuri sana, lakini hao unaowaambia sasa, mh!
For the first time mimi nimeona maajabu ofisa wa ngazi ya juu wa usalama akijitokeza hadhara kufanya PR ya kutokuhusika kuiba kura. Image ya kampuni mfano ikituhumiwa kwa bidhaa feki kinga yake ni kuleta bidhaa bora ili kulinda image yake. Na kama imechafuliwa ni kudai fidia. Chombo kama hiki kama kilikuwa hakihusiki walitakiwa kumkamata Dr. slaa na kumshtaki. kukaa kimya na kutoa press release sanasana iliwasaidia watu kuiona sura ya kigogo yule. Ajabu mbona mambo ya ajabu? au mi ndo sielewi?
Ndugu sio kwamba kila agent wa TISS ni undercover agent wengine niwatumishi wa kawaida ambao kutambulika sio vibaya mfano director wa cia ni General David Howell Petraeus aliye jitokeza wakati ule nikiongozi ambaye lazima ajulikane mfano generali kombe alikuwa mkurugenzi pale tena kwakuteuliwa hadharani.For the first time mimi nimeona maajabu ofisa wa ngazi ya juu wa usalama akijitokeza hadhara kufanya PR ya kutokuhusika kuiba kura. Image ya kampuni mfano ikituhumiwa kwa bidhaa feki kinga yake ni kuleta bidhaa bora ili kulinda image yake. Na kama imechafuliwa ni kudai fidia. Chombo kama hiki kama kilikuwa hakihusiki walitakiwa kumkamata Dr. slaa na kumshtaki. kukaa kimya na kutoa press release sanasana iliwasaidia watu kuiona sura ya kigogo yule. Ajabu mbona mambo ya ajabu? au mi ndo sielewi?
Wadau.
NIMEKAA nikitafakari utendaji wa idara yetu ya Usalama wa Taifa. Hii ni taasisi muhimu sana kwa usalama wa nchi na wananchi wake, nchi zote idara hii ina heshima kubwa ndani ya jamii.
Kwa miaka mingi tangu uhuru wan chi yetu imekuwa na taasisi ya Usalama wa Taifa iliyo imara. Japokuwa mengi mabaya yalifanywa kipindi hicho na idara hii, lakini muktadha wangu naujenga kuhusu Hadhi na Heshima ya idara hii nyeti.
Hivi karibuni Usalama wa Taifa (idara) imeingia katika misukosuko kadhaa na wananchi wakiwemo wanasiasa. Mifano michache ni:
- Mwaka 2010 baada ya uchaguzi, aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema Dr Slaa alitoa shutuma za waziwazi kwa idara ya Usalama wa Taifa kuhusu kuhusika na wizi wa kura na kuingilia mchakato mzima wa uchaguzi ili kuipendelea CCM. Siku chache baadae Afisa mmoja wa Usalama wa Taifa alitoa taarifa kwa vyombo vya habari AKIKANUSHA.
- Tukio la Dr ulimboka limeiingiza idara ya Usalama wa Taifa tena ikiwataja moja kwa moja maafisa wake kutoka Ikulu, hakuna maelezo ya kutoka toka Ikulu kwenye hili
- Mbunge wa chadema (aliyevuliwa) Mh. Godbless Lema alitoa tuhuma kwamba hukumu ya kumvua ubunge ilitokana na maagizo ya Ikulu (Usalama wa Taifa ndio wahusika)
- Dr Slaa/ Mnyika wametoa shutuma za waziwazi wakiwataja maafisa wa Usalama wa Taifa kutaka kuwadhuru kwa staili mbalimbali
Hoja yangu
Idara hii ni muhimu sana, tena yenye heshima na hadhi kwa jamii, ifanye kazi ya kuhakikisha nchi iko salama ili matukio yanayoonyesha udaifu wa mfumo wa kuilinda nchi yetu yasitokee. Mfano Waethiopia wanavuka mpaka na kufia Dodoma katikati ya nchi, je wangekuwa maadui nchi ingesalimika? Je meli zetu zinapata ajali kila mara hakuna hujuma? Madini yanaibiwa na wahujumu uchumi wao wanafanya nini?
Rai yangu kwa usalama wa taifa ni kutoa kipaumbele maslahi ya Taifa sio kulenga kuwaua viongozi wa upinzani (kama kweli madai ya Dr Slaa)
Nakubaliana na wewe mkuu,wafanye kazi kwa maslahi ya Taifa.
Mawazo ni mazuri sana, lakini hao unaowaambia sasa, mh!
For the first time mimi nimeona maajabu ofisa wa ngazi ya juu wa usalama akijitokeza hadhara kufanya PR ya kutokuhusika kuiba kura. Image ya kampuni mfano ikituhumiwa kwa bidhaa feki kinga yake ni kuleta bidhaa bora ili kulinda image yake. Na kama imechafuliwa ni kudai fidia. Chombo kama hiki kama kilikuwa hakihusiki walitakiwa kumkamata Dr. slaa na kumshtaki. kukaa kimya na kutoa press release sanasana iliwasaidia watu kuiona sura ya kigogo yule. Ajabu mbona mambo ya ajabu? au mi ndo sielewi?