Rai yangu Fupi Kwa Rais Samia

Rai yangu Fupi Kwa Rais Samia

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2016
Posts
710
Reaction score
1,365
Kwako MH Rais Wetu MH Samia S Hassan
Awali ya yote pole Sana na majukumu ya Kitaifa ya kila siku

Nikuombe Sana MH Rais ukipata muda uwe na Mkutano Mkuu wa Kitaifa na Wananchi wako,Iwe Dar es salaam, Dodoma au Zanzibar

Agenda kuu itakuwa moja Tu,

Kusikiliza maoni ya Wananchi na kuboresha mapato kwenye Halmashauri, Manispaa TRA na Vyanzo vyote vya mapato

Kuna Taasisi kama TRA au Halmashauri Serikali inapoteza mapato mengi,Kwa uzembe na rushwa iliokithiri

Nikuombe Sana tafuta muda wa siku tatu mfululizo kukaa na Wananchi na kusikiliza maoni ambayo kwayo yatasadia Serikali kuongeza Vyanzo vya mapato

TRA, Halmashauri zote,manispaa na Taasisi zote ziwepo kwenye Mkutano huo

Naamini MH Rais kupitia Mkutano huo utajifunza vitu vingi lakini zaidi Serikali kwenda kuongeza mapato baada ya Mkutano huo

Najua MH Rais Una majukumu mengi ya Kitaifa lakini nikuombe utenge muda wote kwaajili ya hili Jambo muhimu la Kitaifa

Natanguliza Shukrani

afredrick59@gmail.com
 
🤣🤣🤣 Unadhan hawajui wanacho kifanya basi .
 
Aliunda Tume na ipo na inafanya kazi ila kuna watu huwezi kuwagusa kwenye kodi, wana mizizi mirefu. Ukienda kudai kodi chain yake inarudi hadi kwa mkuu wa nchi au ma Concord wa chama Tawala. So wewe kama mwananchi wa kawaida na unauwezo wa kukwepa Kodi wewe kwepa tu, kama ni ofisa na umepata mwanya wa kula Rushwa kula tu mpaka pale nchi itakapoendeshwa na watu wenye akili timamu, wenye kumaanisha wanayo ongea, sio hawa waliodondokewa na zali la mentali.

Kama lugha haikupigi chenga soma hapa
 
Back
Top Bottom