ALECKS MBISE
New Member
- Aug 25, 2015
- 3
- 1
BARUA YA WAZI KWA MAWAKALA NA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI KOTE NCHINI.
Kwanza nawapongezeni sana kwa Kuchaguliwa/kuteuliwa kushika nafasi hii muhimu sana ya maamuzi ya Wananchi juu ya Mustakabali wa Maisha yao na Taifa lao kwa ujumla.
Napenda mtambue ya kuwa mmepewa dhamana kubwa sana na Taifa linawategemeeni ninyi kulinda na kusimamia haki bila kupendelea upande wowote ama bila kupokea shinikizo la namna yoyote lenye lengo la kupindisha ukweli au kutotenda haki.
Nchi itakuwa salama kama Mkijitambua na Kutambua dhamana mliyopewa, Kusimama kwenye nafasi zenu kikamilifu Kulinda, Kutenda na Kusimamia haki. Kumbukeni pia kuwa kinyume ha kufanya haya kunaweza kuliingiza Taifa kwenye machafuko makubwa.
Natoa Rai Kwa Mawakala na Wasimamizi wote wa Uchaguzi Tanzania nzima;
Tambueni ya kuwa mnaenda kusimamia na kulinda maslahi ya Watanzania, mnaenda kulinda na kusimamia maamuzi ya maskin wa Taifa hili, mnaenda kusimamia vilio vya wamama wajawazito wanaokosa huduma bora za afya , mnaenda kusimamia vilio vya vijana wasiokuwa na ajira, mnaenda kusimamia vilio vya watu juu ya Elimu bora, Maisha bora, Huduma za afya, huduma za maji, Umeme, Barabara, Kilimo lakini zaidi ya yote Mnaenda kusimamia na kulinda maamuzi ya Wanyonge wa Taifa hili Kuhusu Umaskini,
Hivyo ninawaombenni sana kwamba KUWENI WAAMINIFU KWA MAAMUZI YA WATANZANIA, msikubali kwa namna yoyote kurubuniwa kwa Kiasi chochote ha fedha au mali ama aina nyingine yoyote ya hongo Mkauza MAAMUZI YA WATANZANIA, Maana kwa kufanya hivyo siyo tu kwamba unahatarisha maisha yako lakini pia unajiwekea LAANA kubwa Kwenye jamii na Kizazi chako na kubwa Zaidi Umekubali na Kuruhusu Watanzania ukiwemo wewe waendelea kuwa Maskini, kukosa huduma za afya, Maji, Umeme, Barabara, Kukosa elimu bora na Vijana kuendelea kukaa bila ajira.
Nendeni Mkatimize kusudi kwa kusimamia Haki, Msiogope vitisho, Muwe majasiri katika Kipindi hiki Muhimu sana cha Mabadiliko.
Mungu na Awe Nanyi, Amen.
Mbise,(2015).
1731hrs.