Raha ya Mapenzi Kupendwa sio kujipendekeza

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,859
Kapo ka hulka kamezuka siku hizi kwenye muundo wa njia za kuanzisha mahusiano.Wanawake wa leo si wale tuliowajuwa enzi zile.Kwanza wamekuwa wepesi kung'oleka kirahisi sana.Miaka ile papuchi ilisotewa kweli kweli.

Pili wengi wamefanya mapenzi yamekosa ladha yake halisi niijuwayo,Wanawake wengi sasa hivi hawasubiri kutongozwa,Wengi hujipendekeza kwa wanaume (Kujilengesha) na wakitupiwa nduano fasta washaitika kwa herufi kubwa"SAWA".

Haya ni maradhi,Na ndio uchangia mahusiano ya siku hizi hayadumu,Tulieni mtongozwe.Tuangaisheni angalau kidogo tujione nasi kuna kitu tulisotea.Hata hela ukizipata ghafla ghafla nazo uwezekano wa kuyenyuka kwa kasi ni mkubwa.

Ni tofauti na yule aliyezisotea zikaingia kidogo kidogo huwa zinadumu mfukoni.Ndivyo ilivyo hata kwenye PENZI likiwa la ghafla nalo hufa ghafla pia.

Badilini tabia mambo ya kujirahisisha na kujipendekeza kwa mwanaume ili akutongoze ni janga kuu kenyu mabinti wa kileo.

Raha ya Mapenzi kupendwa sio kujipendekeza.Ushauri wa bure badilini taabia.
 
Mwanamke alie nisotesha nikimpata atulie,akizingua huwa nna hasira nao. Namumwaga faster naona kama analeta mashauzi
 
Mwanamke alie nisotesha nikimpata atulie,akizingua huwa nna hasira nao. Namumwaga faster naona kama analeta mashauzi
Alikusotesha,Huwa kapo kanidhamu huongezeka lakini.
 
Tatizo wakikataa sana na umri ukienda soko Lao linaisha afu hatuwaoi,,,tungekuwa sserious kuoa hata wawilwawil kwa men mmoja wasingekuwa warahis hivo
 
hata Mimi hua nawaza hivyo hivyo lakn akili nyingine inaniambia nao wana haki kwa sabab umri unaenda, wana moyo pia, hulazimishwi kukubali. Mimi mwenyewe hua nakutana na hizo issue endapo sijampenda namkataa kisaikolojia ili nisimkatshe tamaa kujaribu kwingine ila nikimpenda nitampa nafas na kutreat normal.Nadhan kuna waliojarbu na wamependwa na maisha yameenda cz maisha hayana formula
 
Mmh naona leo kila kidume kitasema kinapenda " usinikubali haraka haraka ", mnataka mzungushwe eti. Sasa nimeona mtu ananifaa jamani ( sijakurupuka ), nilete mapozi ya nini afu akighairi nijifanye nalia lol. ( Kidding )

Haya mambo hayana SI unit, kuna watu wamekutana within a short time na mambo yao yapo freshhhh, wengine yamebuma. Na kuna wengine wamezungushana weee wakaja wakadumu but wengine wakapigana vibuti vya toilet paper. Ni kuomba tu Mungu upate mtu sahihi na kuweka misingi sahihi basi. Afu kumsoma mtu hakuna fixed time, kuna package zinakuja as a whole jamani so unakuta unazielewa mapema teh. Inapohitajika basi utatumia muda mrefu pia kumuelewa mtu. Ila make sure kwa kiasi fulani unamfahamu mtu kabla ya kusema "YES"
 
Back
Top Bottom