Raha ya furaha ndani ya mahusiano

ladyfurahia

JF-Expert Member
May 10, 2011
14,753
9,568
Habari zenu,

Natumaini mu wazima mnaendelea vyema na pilika za maisha ya kila siku leo mabestito nawaletea somo maridhawa la Raha ya furaha inayodumisha ndoa na uchumba na hata mahusiano kiujumla.

Ukitaka kufurahia maisha ya mahusiano basi pawe na furaha baina yenu pasiwe na matengano wala kuoneana kijiba cha roho, wala kuwa na chuki baina yenu hamtafurahia ndoa yenu wala hamtakchangamka kwenye ndoa yenu au mahusiano yenu kama hakutakuwa na furaha.

HEBU TUANGALIE SIRI YA NDOA NI NINI?

A) URAFIKI MWEMA WA MWANZO WA MAHUSIANO

Siri ya kudumisha ndoa yenye furaha ni pamoja na kumuoa au kuolewa na mtu ambaye ni rafiki yako. Kwa maana nyingine urafiki mwema hupelekea kuwa na ndoa yenye furaha baadaye.Mnaweza kuishi kama marafiki mkicheza na kufurahi kuwa pamoja muda wote. Msitegemee kuwa tendo la ndoa pekee ndilo lijenge ndoa yenu hapo mtakuwa mnajidanganya, fikiria kama ikitokea kwa bahati mbaya mmoja wenu akafanyiwa upasuaji utakao pelekea kutofanya tendo la ndoa je mtaendelea kuifurahia ndoa yenu au ndio mtaishia hapo?. Hakikisha hukati mawasiliano na mke au mume wako, likitokea jambo linalowakwaza, kaeni ninyi wawili mlimalize.

Hakikisheni mnadumisha upendo wenu wa kwanza mlio anza nao. Kumbuka ndoa ni kitu kigumu kinahitaji kila mmoja kujitoa kikamilifu kwa mwenzake pamoja na kumuona mwenzake ni wamuhimu saana kwake.

B) KUELEWANA KATI YENU
Mahusiano au ndoa iliyo njema ni ile ambayo wanandoa au wapenzi watakuwa naa maelewano yaliyo mema yasioyo na rabsha au yale ambayo mmoja atataka asikilizwe yeye hata kwa kitu kisichoeleweka basi mwenzio amsikilize tu la hasha bali ni pale ambapo wenzi watakuwa wanaelewena kwa kila jambo kwa umoja na upendo zaidi.

C) USIKATE MAWASILIANO YA MWANZO
Kumbuka siku unakutana na mchumba wako kwa mara ya kwanza mlielewana kwa njia ya mawasiliano , hivyo bila mawasiliano mazuri na mke au mume wako fahamu kwamba ndoa yenu iko kwenye matatizo. Kuongea pamoja, kuelezana pamoja kile ambacho kila mmoja anakihitaji katika maisha yenu ya ndoa huleta maelewano mema kati yenu. Ni kweli kwamba kadri ambavyo mnavyozidi kuishi pamoja mawasiliano yaweza kupungua kwa sababu ya kuzoeana saana lakini kamwe msiruhusu kabisa mawasiliano kukatika. Mawasiliano mema kati yenu ni muhimu katika kuelewa hitaji la mwenzako na huleta furaha katika mahusiano yenu. Mawasiliano ni muhimu, tumia maneno mengi zaidi kuwasiliana na Yule uliyemchagua kuishi naye japo vitendo ni muhimu zaidi kama kumshika mkono, kumkumbatia, kumvalisha, kuvaa nguo wewe mwenyewe nguo nzuri, jipulizie pafumu ile ambayo mchumba wako anaipenda, mpe zawadi japo ni ndogo na za kawaida, vitu hivi huboresha saana mawasiliano ya wana ndoa.

D) UCHESHI NA UKWELI ZAIDI KWA MWENZAKO
Moja ya kitu muhimu saana katika kuwa na familia au ndoa bora ni ucheshi kwa wana ndoa. Ni vigumu sana kubaki na hali ya kufurahi na kucheka pamoja lakini mnaweza kufanikiwa katika hili kwa kutembelea wote katika maeneo mapya kwa pamoja mkiwa wenyewe tu wewe na mume ama mke wako. Kuwa muwazi na mkweli ni msingi muhimu saana kwa wanandoa, hakikisha unakuwa mkweli kwa mke au mume wako hiyo itawafanya muaminiane wote na ndoa yenu itakuwa ni ya furaha siku zote.

E) MTHAMINI MWENZAKO AU MWENZI WAKO
Ili kila mmoja awe na amani katika ndoa ni lazima kila mmoja awe na mchango sawa katika mahusiano. Usioneshe kuwa wewe ni bora kuliko mwenzi wako hii ita mfanya mwenzako ajisikie hana uhuru. Hii ita hafifisha mahusiano yenu kama mke au mume.

F) SAMEHE NA KUSAHAU KABISA.
Wana ndoa wanaofanikiwa katika maisha yao ya ndoa ni wale wanao pokea na kutoa msamaha. Ni wale wanao samehe na kusahau kabisa makosa ya wapenzi wao. Wakati wanapofanya makosa ambayo yanawaumiza wapenzi wao, wao wana omba msamaha. Hivyo kusameheana ni jambo la muhimu saana katika mahusiano.

G) KUVUMILIANA NINYI KWA NINYI.
Mahusiano ya wanandoa wanaofanikiwa kuishi muda mrefu wakiwa nafuraha daima ni wale wanaovumilia hali zote za maisha. Mfano wakati wa magonjwa, wakati wa utajiri, wakati wa umaskini, wakati wa afya njema. Kama wanandoa wataweza kuvumiliana katika hali zote hizi basi wataishi kwa furaha kwa sababu watakuwa wamezipitia nyakati zote hizi, hivyo kila mmoja atamuona mwenzake ni muhimu zaidi.

Hayo ni machache ambayo ni muhimu kuizingatia ili kudumisha RAHA ya furaha ndani ya mahusiano yenu.Niwatakie baraka kwenye mahusiano yenu na mzidi kujifunza kwa wengine waliokuwa mfano

Wasalaam;

Ladyf

cc: Mtambuzi (nimekumissije baba ngina kuja hapa), mwallu, Lady doctor, charminglady,
KakaKiiza, Mentor, Husninyo, Asprin, LiverpoolFC, Heaven on Earth, valentine, Passion Lady, Watu8, Nyani Ngabu, mshana jr, Paloma, sister, Madam B, Ben Mugashe, Tarime one, Tarime one NA MARAFIKI ZANGU WENGINE JONGEENI HAPA
 
Habari zenu

Natumaini mu wazima mnaendelea vyema na pilika za maisha ya kila siku leo mabestito nawaletea somo maridhawa la Raha ya furaha inayodumisha ndoa na uchumba na hata mahusiano kiujumla.

Ukitaka kufurahia maisha ya mahusiano basi pawe na furaha baina yenu pasiwe na matengano wala kuoneana kijiba cha roho, wala kuwa na chuki baina yenu hamtafurahia ndoa yenu wala hamtakchangamka kwenye ndoa yenu au mahusiano yenu kama hakutakuwa na furaha

HEBU TUANGALIE SIRI YA NDOA NI NINI?

A) URAFIKI MWEMA WA MWANZO WA MAHUSIANO

Siri ya kudumisha ndoa yenye furaha ni pamoja na kumuoa au kuolewa na mtu ambaye ni rafiki yako. Kwa maana nyingine urafiki mwema hupelekea kuwa na ndoa yenye furaha baadaye.
Mnaweza kuishi kama marafiki mkicheza na kufurahi kuwa pamoja muda wote. Msitegemee kuwa tendo la ndoa pekee ndilo lijenge ndoa yenu hapo mtakuwa mnajidanganya, fikiria kama ikitokea kwa bahati mbaya mmoja wenu akafanyiwa upasuaji utakao pelekea kutofanya tendo la ndoa je mtaendelea kuifurahia ndoa yenu au ndio mtaishia hapo?. Hakikisha hukati mawasiliano na mke au mume wako, likitokea jambo linalowakwaza, kaeni ninyi wawili mlimalize.

Hakikisheni mnadumisha upendo wenu wa kwanza mlio anza nao. Kumbuka ndoa ni kitu kigumu kinahitaji kila mmoja kujitoa kikamilifu kwa mwenzake pamoja na kumuona mwenzake ni wamuhimu saana kwake.

B) KUELEWANA KATI YENU

Mahusiano au ndoa iliyo njema ni ile ambayo wanandoa au wapenzi watakuwa naa maelewano yaliyo mema yasioyo na rabsha au yale ambayo mmoja atataka asikilizwe yeye hata kwa kitu kisichoeleweka basi mwenzio amsikilize tu la hasha bali ni pale ambapo wenzi watakuwa wanaelewena kwa kila jambo kwa umoja na upendo zaidi.

C) USIKATE MAWASILIANO YA MWANZO

Kumbuka siku unakutana na mchumba wako kwa mara ya kwanza mlielewana kwa njia ya mawasiliano , hivyo bila mawasiliano mazuri na mke au mume wako fahamu kwamba ndoa yenu iko kwenye matatizo. Kuongea pamoja, kuelezana pamoja kile ambacho kila mmoja anakihitaji katika maisha yenu ya ndoa huleta maelewano mema kati yenu. Ni kweli kwamba kadri ambavyo mnavyozidi kuishi pamoja mawasiliano yaweza kupungua kwa sababu ya kuzoeana saana lakini kamwe msiruhusu kabisa mawasiliano kukatika. Mawasiliano mema kati yenu ni muhimu katika kuelewa hitaji la mwenzako na huleta furaha katika mahusiano yenu. Mawasiliano ni muhimu, tumia maneno mengi zaidi kuwasiliana na Yule uliyemchagua kuishi naye japo vitendo ni muhimu zaidi kama kumshika mkono, kumkumbatia, kumvalisha, kuvaa nguo wewe mwenyewe nguo nzuri, jipulizie pafumu ile ambayo mchumba wako anaipenda, mpe zawadi japo ni ndogo na za kawaida, vitu hivi huboresha saana mawasiliano ya wana ndoa.

D) UCHESHI NA UKWELI ZAIDI KWA MWENZAKO

Moja ya kitu muhimu saana katika kuwa na familia au ndoa bora ni ucheshi kwa wana ndoa. Ni vigumu sana kubaki na hali ya kufurahi na kucheka pamoja lakini mnaweza kufanikiwa katika hili kwa kutembelea wote katika maeneo mapya kwa pamoja mkiwa wenyewe tu wewe na mume ama mke wako. Kuwa muwazi na mkweli ni msingi muhimu saana kwa wanandoa, hakikisha unakuwa mkweli kwa mke au mume wako hiyo itawafanya muaminiane wote na ndoa yenu itakuwa ni ya furaha siku zote.

E) MTHAMINI MWENZAKO AU MWENZI WAKO

Ili kila mmoja awe na amani katika ndoa ni lazima kila mmoja awe na mchango sawa katika mahusiano. Usioneshe kuwa wewe ni bora kuliko mwenzi wako hii ita mfanya mwenzako ajisikie hana uhuru. Hii ita hafifisha mahusiano yenu kama mke au mume.

F) SAMEHE NA KUSAHAU KABISA.

Wana ndoa wanaofanikiwa katika maisha yao ya ndoa ni wale wanao pokea na kutoa msamaha. Ni wale wanao samehe na kusahau kabisa makosa ya wapenzi wao. Wakati wanapofanya makosa ambayo yanawaumiza wapenzi wao, wao wana omba msamaha. Hivyo kusameheana ni jambo la muhimu saana katika mahusiano.

G) KUVUMILIANA NINYI KWA NINYI.

Mahusiano ya wanandoa wanaofanikiwa kuishi muda mrefu wakiwa nafuraha daima ni wale wanaovumilia hali zote za maisha. Mfano wakati wa magonjwa, wakati wa utajiri, wakati wa umaskini, wakati wa afya njema. Kama wanandoa wataweza kuvumiliana katika hali zote hizi basi wataishi kwa furaha kwa sababu watakuwa wamezipitia nyakati zote hizi, hivyo kila mmoja atamuona mwenzake ni muhimu zaidi.

Hayo ni machache ambayo ni muhimu kuizingatia ili kudumisha RAHA ya furaha ndani ya mahusiano yenu.
Niwatakie baraka kwenye mahusiano yenu na mzidi kujifunza kwa wengine waliokuwa mfano

Wasalaam;

Ladyf

cc: Mtambuzi (nimekumissije baba ngina kuja hapa), mwallu, Lady doctor, charminglady,
KakaKiiza, Mentor, Husninyo, Asprin, LiverpoolFC, Heaven on Earth, valentine, Passion Lady, Watu8, Nyani Ngabu, mshana jr, Paloma, sister, Madam B, Ben Mugashe, Tarime one, Tarime one NA MARAFIKI ZANGU WENGINE JONGEENI HAPA
Ningeomba na mimi uwe unaniunganisha na list ya hao ulio wa cc,acha ubaguzi Lady furahia wa Mabibo.
 
Back
Top Bottom