Raha na karaha za WhatsApp

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Ndoa ya shost ina miaka mitano sasa, kumbe kuna kigori kinamkosesha raha mume wake, mume amesharusha ndoana mtoto anatoa nje, siku ya siku mtoto ameingia line.

Mume mate yalimtoka, akifikiria alivyohangaika kurusha ndoana, basi akapanga mpango wa kujimilikisha kigoli japo kwa siku tatu. Ofisini alichukua likizo ya dharura, nyumbani akamuaga shost anakwenda Mwanza kikazi.

Alijificha mjini hapahapa, kwenye machimbo ambayo ni nyumba ya kiongozi mmoja wa serikali ameijenge kama retirement home hizo siku zijazo, ni hekalu na kwasasa kwasababu hajahamia, ameamua kuifanya rest house.

Wenye pesa zao wengi huenda hapo kufanya yao wasiotaka yajulikane, kwani wafanyakazi kuanzia mpishi, bar manager na house keeper wote ni Wakenya. Wageni wengine wengi ni raia wa kigeni, kwani sehemu yenyewe malipo ni kwa dola za kimarekani.

Mume ameingia na kigori kujiachia kwa raha zao, kumbe bwana mmoja wa wahudumu ni binamu wa shost, si unajua kuna wale binamu ambae mama yake na baba yako ni binamu, kizungu wanaitwa "2nd cousin".

Binamu anamfahamu shemeji yake kwani alimuona siku ya harusi, lakini hana ukaribu nae sana. Baada ya kumuona anajivinjari na kigori, basi binamu alitafuta number ya simu ya binamu akawa anawalia timing anapiga picha.Mara wako kwenye swimming pool, wanalishana dining, wameshikana mikono wanatembea kwenye garden, basi vurugu tupu.

Binamu alitafuta number ya simu ya mke wa jamaa,akampigia simu kujitambulisha, na kumueleza kinachoendelea na picha akamtumia kwenye whatsapp.

Shost alipopata zile picha ngachoka. Alitafuta mtu akamuomba apige simu kwa secretary kazini kutaka kuongea na fulani, secretary akajibu boss amepata dharura ya kifamilia lakini atakaua ofisini Jumatatu. He shost ndio anagundua kumbe Mwanza ilikua danganya toto.

Baada ya maraha, wakaagana vizuri, mume akaenda kutafuta sato na sangara mjini, kawapeleka nyumbani, akimkumbatia mkewe jinsi alivyomkumbuka.

Shost ananihadithia hasira zilimpanda hakujua afanye nini, lakini wakati anasubiri uamuzi na kichwa chake, alimpikia mume wake chakula kizuri tu.

Wanafuga mbwa, alichukua sahani akawapakulia mbwa chakula wakala, wakailamba basi shost hakuisafisha ile sahani, akampakulia mumewe chakula kwenye sahani ile ile. Jamaa alipokua anakula kidogo moyo wake ulipata faraja,lakini hajajua achukue hatua gani bado.
 
Safi, vipi umeonana na Shigongo leo?
 
Story zako, tamu lakin uhalisia mdgoo
 
Ndio maana kuna watu wanakufuru na kusema wanawake ni Mashetani.
Ndio nini sasa hii?
Hata nikikukosea nini nikijua moja ya adhabu ulizonfanyia ni hii,
Lazima namimi nitengeneze Kichuri kwa Damu yako.
...mbavu zako.
 

Naona binamu hakula kiapo cha maadili ya kazi
 
Ndio maana kuna watu wanakufuru na kusema wanawake ni Mashetani.
Ndio nini sasa hii?
Hata nikikukosea nini nikijua moja ya adhabu ulizonfanyia ni hii,
Lazima namimi nitengeneze Kichuri kwa Damu yako.
...mbavu zako.

Myafanye nyie tukifanya sie tumekua mashetani!
 
Dah aise patamu hapo jamaa naye shidaa anampelekea hao sangara na sato kama ushahidi kuonesha jamaa kweli alienda mwanza
 
Myafanye nyie tukifanya sie tumekua mashetani!
Mi nishasema na ninamaanisha.
Kwani tangia lini mwanamke akawa na kauli mbele ya mwanamme?
Taka ustake yapo mambo wewe mwanamke huwezi kushindana na mwanamme.
Na je wewe unadhani kosa alilolifanya linahusiana na kulishwa denda la Mbwa?
Mi nitatengeneza na supu ya kongolo zake jamani.
 

Ile kauli ya wanawake tunataka usawa ulishaisikia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…