GE2025 Ragi Samwel ajitosa kugombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga

GE2025 Ragi Samwel ajitosa kugombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na aliyewahi kuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), Ragi Samwel , amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga kupitia tiketi ya CCM.

Samwel alipokea fomu hiyo leo, Juni 30, 2025, na kukabidhiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Sylvester Yeredi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Ragi alisema amejiamini na kuona kuwa anatosha kuwatumikia wananchi wa Ukonga na kuchangia katika kuleta maendeleo ya kweli ndani ya jimbo hilo.

Soma Pia: Uzi maalum wa wanaotia nia kugombea Ubunge Uchaguzi Mkuu 2025

Ameongeza kuwa endapo atateuliwa, ataomba ushirikiano wa wananchi ili kushinda kwa kishindo na kuendelea kumsapoti Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuleta maendeleo kwa Watanzania.
 
Back
Top Bottom