Rage: Kifo cha Samuel Sitta ni pigo kwa klabu ya Simba SC

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
1478522976956.jpg
Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba SC Aden Rage, amesema kifo cha Spika wa bunge mstaafu Samwel Sitta ni pigo kwa wapenzi wa klabu ya hiyo kwa kuwa ndiye aliyeshiriki kuitunga katiba ya klabu hiyo

Akizungumza leo Jumatatu Rage amesema huwezi kutaja katiba ya klabu ya Simba bila kutaja jina la Sitta

Rage amesema Sitta wakati wa uhai wake alikuwa mwanachama na mpenzi mkubwa wa klabu ya Simba SC

Amesema kuna kipindi hata jezi za klabu hiyo zilikuwa zinafuliwa nyumbani kwake

Amesema Sitta ametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya klabu hiyo ambayo mengine ni vigumu kuyataja.

Chanzo : Mwananchi
 
rage unafikiri watu wanalala?wanafunga na kuomba alichofanya sita na wenzake kinajulikana njoo uchaguzi uliopita kilichofanyika kinajulikana
 
Mshtuko wa kufungwa Jana simba ndy imepelekea kifo chake au? Pumzika sehemu unayostahili.....ameen
 
Mshtuko wa kufungwa Jana simba ndy imepelekea kifo chake au? Pumzika sehemu unayostahili.....ameen
Si anaelezea mchango wake katika klabu.. ama kufungwa ni ile ile tu moto wa ushindi unaendelea tu
 
Kama ilikuwa inamtegemea 6 bora ifungwe tu.

Nyie wazee (rage) badilikeni, zile zama za kupitishia propaganda zenu kwenye michezo hazina nafasi.
Katiba yetu itamwandama mpaka akome.
 
Simba ndio nini?matimu ta ajabu ajabu yanayorudisha nyuma soka la Tanzania
 
TFF ndo walodishao shoka la Tanzania, vilabu kosa lao ni lipi..!?
tff inaziogopa simba na yanga,hazikawii kutishia kuhamia ligi ya zenj,pia mechi yao moja inalipa marefa ligi nzima,watendaj wa tff weng ni watu wa timu hzi,ngumu kwenda nao kinyume
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom