katika kile kinachoweza kujulikana kama ni kuzidiwa na madaraka, mbunge wa jimbo la tabora mjini Alhaj Aden Ismail Rage leo ameumbuka katika kikao maalumu cha chama cha mpira wa miguu mkoa wa tabora TAREFA baada ya siku chache zilizopita kutangaza kujiuzuru na leo kugoma kuwa maamuzi hayo yalifanyika kimakosa na hata pale wajumbe wa kikao walipotaka kuchangia hoja juu ya migogoro ya soka mkoa wa Tabora Rage aligoma kata kata kuruhusu mjumbe yeyote kuongea na kusema kuwa hakuna kikao, hali iliyowalazimu wajumbe kutoka nje ya kikao na kususia chai na hata posho zaidi angalia kipindi cha michezo ITV,Cten na TBC leo au kesho asubuhi. baada ya wajumbe kumsusia Rage kikao hicho na kubaki peke yake alitoka taratibu na kutembea kwa mguu kuelekea kwa kwake ambapo si mbali na eneo palipotakiwa kufanyika kikao hicho