Habari za muda huu wadau
Niende kwenye mada .....rafiki yangu Noel alipata kua na mchumba ,mchumba ambae alimrubuni toka akiwa shule ,basi mtoto wa kike akafukuzwa kwao na kwenda kuishi kwa Noel baada ya kumaliza kidato cha nne ,bwana Noel alikua jobless so aliishi mtaani kwa kutanga tanga alifanya kazi ya kufunga ma dish,kujenga na ata kuchambua vitunguu pale sokoni ilimradi mkewe apate kula,haba si haba kidogo alichokipata Noel aliamua kumpeleka mkewe chuo cha ualimu pale singida ,mkewe akaipata elimu na kutunukiwa cheti cha elimu ya msingi....
Noel akona huo ndo muda sahihi wa kumpiga mimba mkewe,akafanya juhudi zote kitandani na kweli Mungu si athumani bibie akaanzapata jiskia kichefu chefu,kutapika na kupata hamu ya kula udongo....akiwa mjamzito habari njema zikawafikia kwamba post za ajira zimetoka na bibie kapangwa kua mwalimu wa elimu ya msingi huko manyoni, furaha ilikua kifani kwa bwana Noel akipita na kujitapa kwa ndugu jamaa na rafiki kwamba hakupoteza pesa zake bure kulipia elimu ya mkewe, akiwa mjamzito mkewe aliripoti kituo cha kazi huku mkoba na bag kabeba Noel .....
bibie akaanza kazi na Noel akarudi singida kuendelea na vijishughuli vyake vya kutafuta riziki ....baada ya miezi 9 kutimu bibie akapata uchungu na kukimbilia hospital, huko akajifungua mtoto ambae ata hivyo hakua riziki....hyo imuumiza sana Noel lakini wote kwa pamoja wakaamini kua kazi yake Mungu haina makosa, baada ya muda kupita bibie akaendelea na majukumu yake ya kazi na mara kwa mara Noel alienda manyoni kumjulia hali mkewe....basi kupita muda kdg Bibie akajikuta kaangukia penzi la boda boda na kamsahau kabisa Noel ,
Noel kaona akipiga simu hazipokelewi ikawa si shida kwake akapanda bus na kwenda manyoni ,huko akampata mkewe aishi kinyumba na bwana boda boda tena penzi lakolea na maskio yameziba nta, Noel akapata kuchanganyikiwa hasa pale bibie alimpomueleza wazi kua wazazi wake wamekataa kata kata wao wawe mke na mume hivyo ameamua kujiopolea bwana mwingine ambae ni Hugo boda boda....akampa Noel nauli na kumshauri arudi singida.....
Noel mwili ukaporomoka kwa mawazo akaona kulipa kisasi ni kuirudia kalamu na karatasi....Noel sasa amerudi shule hilo ndo kaona jambo jema kufanya kutuliza hasira zake.
Vipi we rafki yangu yangekupata ya Noel ungechukua hatua gani???