Ng'wanapagi
JF-Expert Member
- Sep 18, 2013
- 9,125
- 8,644
Nimetumiwa hii taarifa asubuhi kukamatwa kwa rafiki yangu huko kijijini baada ya kuwaliza watu kibao akijidai ni afisa wa jeshi katika kitengo maalumu kilichosambaa nchi nzima kumsaidia Magufuli katika masuala ya usalama na kutumbua majipu.
Akitumia picha aliyotengeneza (Photoshop), kwa kuwa utaperi wake alikuwa anaufanyia vijijini kwa kuwakamata watu mbalimbali hasa wauza pombe za gongo na mnavyofahamu ndugu zangu vijijini hawafahamu chochote kuhusu photo shop.
NAMNA ALIVYOKAMATWA
Baada ya kufanya utaperi wake aliingia bar na kulewa chakari hadi muda wa doria ukafika ndipo akaanza kujikongoja kwenda anakofahamu yeye na hapo walinzi wa kampuni inayolinda wakamkamata na ndipo akaanza kuwatisha kuwa atawaweka ndani kwa kosa la kumkamata mwanajeshi wa jeshi maalumu la raisi!!
Hapo ndipo wakaanza kumhoji ataje vikosi vyote lkn akazidi kuwa mbogo na ndipo akaitwa mwenyekiti wa kijiji kuja kumsikiliza mwanajeshi feki.
Mwenyekiti nayeye alipofika na kuonyeshwa picha akapiga saluti za utii  !! Akatokea jamaa mmoja maana walipomkamata ni karibu na maeneo ya hospital (saa saba usiku) na akamtambua kuwa si mwanajeshi hata darasa la saba hajamaliza. Hadi sasa yuko kituo cha Polisi.
Nilikuwa nae kijijini kama rafiki yangu huku nikiwa sifahamu chochote kuhusu tabia yake ya utaperi hadi leo nilipopewa hii taarifa na wadogo zangu walioko home.