kwetumasoko
JF-Expert Member
- Aug 24, 2016
- 866
- 510
Kuna kesi nimeletewa na rafiki yangu wa karibu sana kuhusu mahusiano yanayoendelea kati yake na mpenzi wake, hivyo anaomba ushauri kutoka kwangu.
Kaniambia kuwa katika mahusiano yao, wamedumu kwa muda wa miaka miwili lakini bado hawajafunga ndoa, hivyo wanaishi tofauti kila mmoja kwake lakini wilaya moja.
Mpenzi wake ni mtu wa kusafirisafiri wilaya mbalimbali kulingana na kazi anayofanya, anaweza kukaa huko field kwa muda wa wiki moja au hata zaidi.
Mara nyingi wamekuwa na mawasiliano mazuri na jamaa kwa muda wote awapo mbali, hata arudipo kutoka huko na mambo mengi wamekuwa wakishauriana kwa pamoja, na vilevile mpenzi wake huyo anaposhauriwa ni mwepesi kupokea ushauri.
Unajua huyo rafiki yangu yeye hanywi pombe ya aina yoyote, isipokuwa huyo mpenzi wake anakunywa pombe, na wakati mwingine hunywa na kulewa! Kwa upande wa pombe akimwambia aache kunywa sana, anamwambia kama unaona nakunywa pombe sana ni afadhali uniache.
Mbali na hapo analalamika kuwa mpenzi wake akienda kulala nyumbani kwake huwa anamwambia hajisikii kabisa kufanya mapenzi, inshort anamnyima kabisa. Ameniambia kuwa amekuwa akimfanyia hivo kwa muda mrefu, na akimhitaji huwa anaenda kulala, lakini mapenzi no. anamkatalia kabisa. Kwa hiyo kaja kwangu analalamika na kuomba ushauri.
Nami nawasilisha kwenu waungwana, niombe ushauri jinsi ya kumshauri huyo rafiki yangu.