Rafiki yangu amehamia CCM, naomba ushauri!

Rafiki yangu amehamia CCM, naomba ushauri!

mwambie aendelee tu kupata riziki yake,lakini ajue wapi kwa kupeleka kura yake ikifika October
 
hadithi yako inatufundisha nini?

Kuna kamanda tulikuwa nae BAVICHA tukipanga mikakati na kuhamasishana juu ya kuimarisha chama, kuongeza makamanda na mambo kibao.

Umepita kama mwezi hivi bila kuonana kwa kuwa nilisafiri. Jana nikakutana na kamanda, amekuwa mpole, amenyong'onyea, hajiamini. Nikampiga kwanza ofa ya samaki na ndizi rost kwenye kibanda umiza. Kidogo akaanza kufunguka kwa wasiwasi,".. Jamaa yangu, nimehamia CCM!" Halafu akatulia kuangalia reaction, sikuonyesha chochote.

Kisha akaendelea "...Wife amejifungua, sina kazi, nimejaribu kila issue inagoma. Hali yangu ni mbaya kiukweli. CCM wamemwaga yale mahela ya wizi, naweza angalau kupona".

Nilisikia tumbo limenivuruga, Nikakosa swali la kumuuliza, ila baada ya muda nikamuuliza, mnamnadi mgombea gani? Mna uhakika wa kushinda? Akasema "Mimi sijui mgombea wala mambo ya kushinda, wao wenyewe wanajua watashindwa, mimi nashabikia tu kila kitu chao."

Mteja wangu wa kuku akanipigia simu, ikabidi niahirishe mazungumzo na kamanda.
Sasa leo tunakutana, jamani nimwambieje?

Naomba ushauri..
 
Hadithi yako inatufundisha kwamba UKAWA njaa tu.Fursa zote zimehodhiwa na wajanja wachache wa kutoka Kilimanjaro.
 
I can't join him,sitaki kuiona CCM madarakani,I will participate in any movement to get rid of this shit!

Muulize tu kichwa kipo wapi na moyo uko wapi!Kama moyo upo CDM mwambie tu ale.CCM Kura CDM.Na pia ahakikishe siri zote za kuhujumu zinafika CDM.Sawa eh
 
Kwa hiyo unataka tukusaidia nini kama hana pesa mwambie aende kwenye ofisi za ccm atasaidiwa aende na huyo mke wake
 
Nashauri kabla hujakutana nae pata kwanza kile kinywaji chenu mtakachokihalalisha october mkiingia madarakani!

Kadhi Mkuu;
Kinywaji kipi hicho, kile cha yule mgombea/Mtia nia ya kugombea wa ccm kuleeee ziwa kule?? Mbona anakipenda kuliko chama chake? Nakuambia akipita, bila hata hiana, atatangaza ccm ikikubali hicho kinywaji.
Angalia usitupe mawe kwenye nyumba za tembe wakati weye yako ni ya viooo.
 
mwambie ale umagambani kura ukawa.

Ushauri mujarabu kabisa, na pia hamasisha wengi. Hiyo ni fedha yetu tumeibiwa kwa njia za EPA, Richmond, meremeta na juzi kati Escrow ati zikaitwa "Tuhela twa mboga". Fedha ikiwa mifukoni mwao ni za kifisadi. Ukipewa ukaweka mfukoni mwako ni Hallal, kula shiba, tarehe 25 Oktoba, kura yako Hallal weka kwa UKAWA tuu. Usipotee njia.
Anayenunua njia ya Ikulu, ataiziba akiwa anaingia, hatoki tena kwa miaka 10 ijayo.
 
Kadhi Mkuu;
Kinywaji kipi hicho, kile cha yule mgombea/Mtia nia ya kugombea wa ccm kuleeee ziwa kule?? Mbona anakipenda kuliko chama chake? Nakuambia akipita, bila hata hiana, atatangaza ccm ikikubali hicho kinywaji.
Angalia usitupe mawe kwenye nyumba za tembe wakati weye yako ni ya viooo.
Wa Kanda ya ziwa yeye anakunywa kivyake na hajatangaza nia ya kukihalalisha akiingia madarakani. Naongelea kile alichopendekeza mtumishi wa Mungu aliyeasi.
 
Usisahau

*****************

Kupiga kura
Diamond Platnumz kategori 3 (tatu) - Best MALE, Best COLLABORATION na Best LIVE and Vanessa 1(moja) -- Best FEMALE

ingia kwa link hii chini

http://mama.mtv.com/voting/


Bonyeza bonyeza VOTE usichoke

******************
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom