Rafiki yangu amehamia CCM, naomba ushauri!

Paul Alex

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2012
Posts
4,344
Reaction score
9,845
Kuna kamanda tulikuwa nae BAVICHA tukipanga mikakati na kuhamasishana juu ya kuimarisha chama, kuongeza makamanda na mambo kibao.

Umepita kama mwezi hivi bila kuonana kwa kuwa nilisafiri. Jana nikakutana na kamanda, amekuwa mpole, amenyong'onyea, hajiamini. Nikampiga kwanza ofa ya samaki na ndizi rost kwenye kibanda umiza. Kidogo akaanza kufunguka kwa wasiwasi,".. Jamaa yangu, nimehamia CCM!" Halafu akatulia kuangalia reaction, sikuonyesha chochote.

Kisha akaendelea "...Wife amejifungua, sina kazi, nimejaribu kila issue inagoma. Hali yangu ni mbaya kiukweli. CCM wamemwaga yale mahela ya wizi, naweza angalau kupona".

Nilisikia tumbo limenivuruga, Nikakosa swali la kumuuliza, ila baada ya muda nikamuuliza, mnamnadi mgombea gani? Mna uhakika wa kushinda? Akasema "Mimi sijui mgombea wala mambo ya kushinda, wao wenyewe wanajua watashindwa, mimi nashabikia tu kila kitu chao."

Mteja wangu wa kuku akanipigia simu, ikabidi niahirishe mazungumzo na kamanda.
Sasa leo tunakutana, jamani nimwambieje?

Naomba ushauri..
 
Mpe hongera kwa mkewe kajifungua, halafu mpe pole kwa kulea mtoto asie wake
 
Mwambie kala bingo...kapata fedha za bure na zitamtokea puani hivi karibuni
 
Mwambie aache tamaa mtoto wa kiume. Alaf kama anaweza em mwambie akuambie kafanyaje kupata hilo dili uje ushare hapa tuzidi jua kiundani kidgo hayo maujanja
 
Mpe hongera kwa kuwa amefuata katiba inachoeleza kuhusu uhuru wa kuchagua.
 
Hawa ni vizuri waondoke sasa hivi coz ni shida tupu kwa baadae
 
km alifulia long time na wife ana tabia km zake ni wazi kwamba hata mtoto anaweza kuwa si wake.Pengine angekula hela ila asifanya kazi ya ccm zaidi ya kuchukua kadi ila kura iwe kwa Upinzani.Ila ni wengi sana wenye akili hizo kwa shida ndogondogo.
 
kwani bavicha msipoongopa hamuwezi kulala?
 
Kuna kamanda tulikuwa nae BAVICHA tukipanga mikakati na kuhamasishana juu ya kuimarisha chama, kuongeza makamanda na mambo kibao.

Umepita kama mwezi hivi bila kuonana kwa kuwa nilisafiri. Jana nikakutana na kamanda, amekuwa mpole, amenyong'onyea, hajiamini. Nikampiga kwanza ofa ya samaki na ndizi rost kwenye kibanda umiza. Kidogo akaanza kufunguka kwa wasiwasi,".. Jamaa yangu, nimehamia CCM!" Halafu akatulia kuangalia reaction, sikuonyesha chochote.

Kisha akaendelea "...Wife amejifungua, sina kazi, nimejaribu kila issue inagoma. Hali yangu ni mbaya kiukweli. CCM wamemwaga yale mahela ya wizi, naweza angalau kupona".

Nilisikia tumbo limenivuruga, Nikakosa swali la kumuuliza, ila baada ya muda nikamuuliza, mnamnadi mgombea gani? Mna uhakika wa kushinda? Akasema "Mimi sijui mgombea wala mambo ya kushinda, wao wenyewe wanajua watashindwa, mimi nashabikia tu kila kitu chao."

Mteja wangu wa kuku akanipigia simu, ikabidi niahirishe mazungumzo na kamanda.
Sasa leo tunakutana, jamani nimwambieje?

Naomba ushauri..

Kwani yeye alikwambia uje utuulize sisi humu JF?
 
km alifulia long time na wife ana tabia km zake ni wazi kwamba hata mtoto anaweza kuwa si wake.Pengine angekula hela ila asifanya kazi ya ccm zaidi ya kuchukua kadi ila kura iwe kwa Upinzani.Ila ni wengi sana wenye akili hizo kwa shida ndogondogo.

Kwani, hivi ruzuku huwa haifiki mikononi mwa BAVICHA?
 
Kuna kamanda tulikuwa nae BAVICHA tukipanga mikakati na kuhamasishana juu ya kuimarisha chama, kuongeza makamanda na mambo kibao.

Umepita kama mwezi hivi bila kuonana kwa kuwa nilisafiri. Jana nikakutana na kamanda, amekuwa mpole, amenyong'onyea, hajiamini. Nikampiga kwanza ofa ya samaki na ndizi rost kwenye kibanda umiza. Kidogo akaanza kufunguka kwa wasiwasi,".. Jamaa yangu, nimehamia CCM!" Halafu akatulia kuangalia reaction, sikuonyesha chochote.

Kisha akaendelea "...Wife amejifungua, sina kazi, nimejaribu kila issue inagoma. Hali yangu ni mbaya kiukweli. CCM wamemwaga yale mahela ya wizi, naweza angalau kupona".

Nilisikia tumbo limenivuruga, Nikakosa swali la kumuuliza, ila baada ya muda nikamuuliza, mnamnadi mgombea gani? Mna uhakika wa kushinda? Akasema "Mimi sijui mgombea wala mambo ya kushinda, wao wenyewe wanajua watashindwa, mimi nashabikia tu kila kitu chao."

Mteja wangu wa kuku akanipigia simu, ikabidi niahirishe mazungumzo na kamanda.
Sasa leo tunakutana, jamani nimwambieje?

Naomba ushauri..
Nashauri kabla hujakutana nae pata kwanza kile kinywaji chenu mtakachokihalalisha october mkiingia madarakani!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom