sio kwamba ni mbovu ila nachoamini linaundwa zengwe ili wakubwa wapate pa kula.
Yah, hapa kuna mzinga mwingine wa kifisadi unatengenezwa hapa!sio kwamba ni mbovu ila nachoamini linaundwa zengwe ili wakubwa wapate pa kula.
hakuna nchi kama hii duniani
hakuna
Wakati Tanzania ikiwa tayari kutaka kuingia vitani dhidi ya Malawi, Ile rada kuu inayotegemewa kwa mambo ya anga, mawasiliano, kijeshi na kutua kwa ndege iliyopoko Dar kwenye uwanja wa zamani wa ndege imeharibika kwa karibu mwezi mzima sasa.
Hii ndio rada iliyonunuliwa kutoka uingereza na kuzaa kashfa ya ufisadi.
Sababu kuu ya kuharibika kwake ni matatizo ya kukatikakatika umeme nchini.
Matengenezo yake yatahitaji vifaa na wataalam kutoka kwenye kampuni ileile ya uingereza uliyotuuzia rada hiyo.
SOURCE: BBC
mkuu hii newz ni kweli hata dg wa mamlaka ya anga amekiri kuwa rada ni mbovu. watu wa ndani wanenitonya kuwa sbb rada ni ya kizamani, kifaa kilichoharibika hakitengenezwi tena na waingereza kwa hiyo kuna uwezekano rada yetu ya bei ghali lakini ya kizamani ikawa ni km pambo tu au tembo mweupe. hii ndo bongoland.
mkuu kwani rada mnayoiongelea ni ile tuliyoshawishiwa na Toni blea aah sore alishawishiwa ANBEN
Mwambie Chenge alete vijisenti vyake irekebishwe!
Hii wiki ya pili
na nadhani mnajua kama BAE SYSTEMS wanataka ma bilioni kuja kuifanyia marekebisho
uzuri rada tuliuziwa na wawekezaji ambao tunawapenda na tunawaona sio matapeli (wazungu)
Ingekuwa tumeuziwa na Waarabu naona kungekuwa kunawaka moto sasa
Kazi kwenu na nchi yenu ya kufikirika
Najua uwanja wa ndege umebadilishwa jina lakini silipendi kulitumia hiyo jina kipya linantia kichefu chefu na naomba uamuzi wangu uheshimiwe