Prof. Ndullu ni mmoja wa manaibu Gavana 2 walioteuliwa mwezi August mwaka huu. Huyu bwana aliondoka Mlimani mwaka 1989 akaenda Nairobi kuwa Executive Director wa African Economic Research Consortium. Baada ya hapo alichukuliwa na World Bank akakaa Bongo for some yrs kabla hajapelekwa DC. Appointment yake ya kuwa Naibu Gavana amepewa akiwa World Bank.
Kuna wanao sema kwamba na yeye ilikuwa aje Tanzania kama alivyoingia Ballali. JK alitaka awe mshauri wa Rais wa maswala ya uchumi, but for reasons best known to himself jamaa ali-punch hiyo post. Watu walioteuliwa kuwa washauri wa Rais wa maswala ya uchumi ni mapendekezo ya Ndullu kwamba anawafahamu na wangefanya kazi nzuri. Watu hao ni Dr. Mpango na Dr. Mwinyimvua. Dr Mpango alikuwa akifanya kazi World Bank Dar, na Dr Mwinyimvua alikuwa akifanya kazi za muda hapo World Bank Dar lakini sehemu yake ya kudumu ilikuwa ni Mlimani.
Wadadisi wa mambo bado wanajiuliza, ilikuwaje akakubali post ya u-Naibu Gavana ilhali alikataa nafasi ya ushauri wa Rais? Wapo wanaosema kwamba alipelekwa hapo ili akasome mazingira kabla ya kuikwaa post ya u-Gavana.
Pamoja na hayo baadhi ya watu wanaotajwa hapo juu hawana sifa za kuwa Gavana. Sheria ya BoT ya mwaka 2006 inasema kwamba mtu kuteuliwa kuwa Gavana lazima awe na uzoefu wa kuwa kwenye senior position kwa muda wa miaka 15 kama sikosei, au awe amefanya kazi kwenye mashirika makubwa ya kimataifa kwa muda wa miaka 8. Kwa hiyo mtu kama Dr. Natu Mwamba sijui kama ana-fit, labda kama watapindisha sheria. Hao wengine waliotajwa wana sifa hizo. Lakini nadhani inabidi tusubiri tuone mwisho wa siku mambo yatakwendaje!