Wewe hujui ni kwanini Mama anapata kura sivyo?
Pia ili tusiende nje ya mada..Then taja sifa za hao viongozi wako vs R.Mengi.
Sifa zinazohitajika kwa rais VS zile alizonazo R.Mengi!
Hapo ndipo nitakapo waweza critics!
Naamini mjadala ndio kwanza unaanza!
Na pia kuna mabadiliko mengi sana ikija kwenye kupima chuki dhidi ya Mengi pale tunapo compare previous times VS the current moment!
Maneno ya busara sana haya mwan TANU!Baada ya kuchoshwa na hizi habari za ufisadi ulivyoshimiri nchini,.Nimeona inabidi watu tuwe optimistic (dini ya masikini)kuwa tupo katika transitional period.
Kama ilivyotokea Russia baada ya Yeltsin kuiuza nchi kwa mafisadi akatokea Putin sasa sijui was gift from sir God au vipi....basi na sisi Tanzania kuna mtu ambaye si famous bali ni mtendaji kazi zaidi ya Sokoine anakuja......you can call me psychic or nimepagawa......lakini naamini (ndoto za mnyonge)hivyo.
kama hatuwezi kujipa moyo au kujidanganya basi tufanye kweli.....Mkuu huenda kidogo nimetoka kwenye mada alkini nipo palepale KIONGOZI ANAYETUFAA
Taabu yetu sisi watanzania ni pale tunapomzulia mtu jambo kama yeye kasema anataka kugombea u press,hii ni hatari sana, mzee wa watu kila kukicha anawafikiria waremavu, wagonjwa na hata kusaidia elimu, leo mmeamua kumkalia kiti moto, si vizuri hata kidogo,
isaya.. you are very right... kama angeonesha nia ya kuutaka Urais basi tungekuwa na sababu kubwa ya kumjadili. Kina Mbowe, Salim, na wengine walionesha nia ya kutaka kuwania Urais... unless kama kuna mtu anajaribu kumshawishi kuwania.. otherwise tunaweza kuwa tunapoteza muda muhimu kweli kumjadili mtu ambaye hajawahi kuonesha nia ya kuutaka Urais.
Nyerere pamoja na mapungufu yake mengi ambayo yamesemwa sana, alijaribu sana kuiheshimu Ikulu. Ni wale waliokuja baada yake ndio wamegeuza nyumba hiyo kuu ya watanzania kuwa genge la biashara na kitovu cha ufisadi.
Hivyo binafsi naogopa kabisa na kutetemeka nikisikia mtu anataka kwenda Ikulu au anataka Urais kwani najiuliza kwanini? Hilo peke yake halinitishi sana lakini inapotokea mtu anatumia mbinde kupata nafasi hiyo basi hofu yangu ya mtu huyo inaongezeka mara 180!
Mtu mwenye akili timamu hatamani kubebesha mzigo huo; mzigo huo atabebeshwa kwa kuombwa na watu wenyewe, hautafuti.
Wakuu tumejadili sana kuhusu watu wenye kufaa kutuongoza wakati huu mgumu si tu nchini mwetu..Bali Barani mwetu Afrika na Duniani kwa ujumla!
Kuna Candidates wengi tu ambao wametajwa!
Is it right to mention R.Mengi for President?