Nini kimekatisha uhai wake.Habari zilizotufikia muda huu mchezaji wa zamani wa team za Taifa, Pan Africa, Yanga, Lawrence Mwalusako amefariki alfajiri hii katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili
====
Alikuwa beki shupavu amezichezea timu kadhaa nchini ikiwemo Waziri Mkuu ya Dodoma, Pan African na Yanga
Mwaka 1986 kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao wa kucheza soka alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuchezea timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ iliyokuwa ikinolewa na Joel Bendela
Alisataafu kucheza soka ya ushindani mwaka 1991 akiwa na klabu ya Pan African alisifika kutokana na aina ya uchezaji wake, wa kumudu kucheza vyema nafasi zote za ulinzi
Mwalusako baada ya kustaafu kucheza soka ya ushindani amejihusisha na uongozi katika klabu kongwe nchini ya Yanga akiwa kama Katibu mkuu wakati wa Mwenyekiti Imani Madega na mara ya pili akikaimu nafasi hiyo mwaka 2012 baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Celestine Mwesigwa kusimamishwa
Nyota huyu baada ya kuachana na kazi za uongozi katika klabu ya Yanga hivi sasa alijikita katika shughuli za kutoa ushauri wa masoko ‘Marketing Consultation’ akifanya shughuli hizo hapa jijini, lakini kwa sababu mchezo wa soka uko kwenye damu yake bado anatoa msaada wa ushauri katika klabu yake ya zamani ya Yanga iliyo na maskani yake makuu mtaa wa Jangwani na Twiga
Ugonjwa ni Siri ya mgonjwa, familia yake na daktari wake...ni Sheria au taratibu za nchi yetuHakukua na sababu ya kueleza alikua anafanya nini kwa sasa.
Watu wanalazimika kujua ni nini kimekatisha uhai wake.
Yanga mnakwama wapi?
During treatment.Ugonjwa ni Siri ya mgonjwa, familia yake na daktari wake...ni Sheria au taratibu za nchi yetu
Muhimbili awalazi wa COVID19. Na yupo kwa mda mrefu pale hospitalAcha hizo...ndiyo nyie mnaosemwa mnasambaza uongo...huyu comrade Alikuwa na matatizo muda mrefu...Tena nimedokezwa Alikuwa amefanyiwa operesheni
Muhimbili hawalazwi wa #covid19 jomba.Halafu toka lini mgonjwa wa #covid19 akafanyiwa upasuaji....Mbona kama unalazimishaDuring treatment.
Sababu ya kifo sio siri ya yoyote.
Corona inakaba koo!
Nadhani kiharusiNi upumuaji tena?
RiP
Wasifu wa marehemu ni pamoja na kilichokatisha uhai wake.Muhimbili hawalazwi wa #covid19 jomba.Halafu toka lini mgonjwa wa #covid19 akafanyiwa upasuaji....Mbona kama unalazimisha
Alicheza miaka ipi ?LAWRENCE MWALUSAKO KWA WATU WENYE UMRI ULIOPEVUKA KAMA SISI, BASI LIKITAJWA JINA HILO TUNAKUMBUKA MBAAAAAAAALI SANAAA. DAAAAH
KAKA YETU AMETUTANGULIA! KWELI DUNIA TUNAPITA TU JAMANI.
Huyu alicheza miaka ipi ?Maana katika kumbukumbu zangu sikuwahi sikia hili jina. Mimi nawakumbuk kina Ken Mkapa,Thom Kipese,Sanifu Lazaro,Kabunda n.k
Hapo nilikuwa bado. Ila yeye itakuwa aliacha mpira before Minziro,sure boy na Abeid Mziba maana hao akili yangu inakumbuka kusikia hayo majina.1985.1989 hiyo uliza kina Abeid Mziba, Fred Felix Isaya Minziro, Joseph Fungo, Sure Boy etc