Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,483
- 167,058
Nina katoto kadogo ka miezi sita,
tangu jana jioni kamekuwa kakisumbuliwa na malaria,
leo asubuhi nimekapeleka lugalo hospitali kwa kuwa ndio hospitali iliyopo jirani na makazi yangu kawe ukwamani.
Mtoto kapimwa na vipimo vinaonyesha kuwa ana vimelea vya malaria.
Cha kushangaza ni kwamba, daktari amegoma kuniandikia dawa anasema eti niende manzese darajani kuna hospitali inaitwa farbec,
hapo ndipo ntapata dawa inayoitwa quinine mixture ambayo hutengenezwa wao wenyewe.
Mi nimeamua kwenda hospitali nyingine kutafuta dawa sahihi ya kutibu malaria.
Maswali yangu machache ni kuwa hiyo quinine mixture inayotengenezwa na hao wauguzi wa manzese, imethibitishwa na nani kuwa ni tiba salama ya malaria?
Je ni yepi madhara kando (side effect) ya dawa hiyo
je ni kweli inafanya kazi?
Je majaribio na tafiti vilifanywa wapi??
Naomba wadau wa afya waitupie macho hospitali hiyo.
Vinginevyo serikali itoe tamko rasmi kupitia wizara yake ya afya.