Qatar Airways route za Dar/KIA analeta mikangafu!

Alipata isolated incident. Hii huwa inatokea kama ndege iliyopangiwa route inakuwa ina matatizo mnaletewa ya dharura...na huwa wanasema.

Nilipanda Boeing 777 ya Qatar kutoka JFK mpaka Doha dah! Siti pana, ndani kuzuri, entertainment safi na chakula cha kueleweka. Hata mimi ukiniambia nichague nitachagua KLM na Qatar always japo na wengine akina BA wapo....

By the way, mashirika ya ndege ya Kimarekani niliyowahi kupanda - Delta, United, NWestern, American...yote hayafai. Viti vimerundikwa, huduma mbovu ikiwemo chakula. Haya kama mtu una vihela afadhali hukoo Business class kama una lisafari lirefu!

Nasubiri siku nikipanda ndege za mashirika ya Asia - Indonesian Airlines, Thai, Korean, Malaysian, Japanese....nasikia wao wako level nyingine kwenye design na hospitality...
20231224_095052.jpg
 
Jamaa huwa hawana Sajesheni boksi?,nadhani haya malalamiko ungehakikisha yanaufikia uongozi wa hilo shirika ungekuwa umetisha sana kwani ungewasaidia wengi!
Ukiingia kwenye website yao na uandike malalamiko yako ndio hakuna zaidi, ukipiga simu inakwenda Doha na huko hakuna msaada wowote, najua watu tunalalamika ukipiga simu ATC ( Air Tanzania )hakuna majibu lakini Qatar ndio wazembe kuliko ATC, ukifika Doha bora ukutane na wa Kenya wanaweza kukupa msaada lakini desk nyingi utakuta wa Hindi na ukitoa Pass ya Tanzania hesabu maumivu
 
Umepata bahati ya kupanda A350, usiombe kupanda Boeing 777 ya Qatar, viti ni vidogo kwa safari ndefu
airport kubwa lakini huduma sio za kuridhisha,
sitoipanda Tena Qatar Airways nipo tayari kuwapa Ethiopia pesa yangu kuliko Qatar, ukiwa na pass ya Tanzania ndio kabisa huthaminiwi,
itakuwa chaguo la mwisho kuchagua Qatar, simshauri mtu kusafiri na Qatar airways

Ethiopia hiihii ninayoijuwa mimi au nyingine. Hata bure hunipandishi.
 
Nimepanda mashirika mengi ila sijaona linalozudi SQ- Singapore airline- hawa Jamaa huduma zao, usafi wao, na chakula ndani ya Ndege ni full masinonda…
Changi airport pia ni safi sana - ni 5 start airport na Kwa kweli- nilitembelea ma super market Yao kujionea tu bila kuwa na nia ya kununua chochote, Ila nilivyotoka nilikuwa na lundo la shopping- hawa wa Singapore wanajua nini maana ya customer services/ care Kwa kweli… inabidi watu wetu wakajifunze huko…
 
Tatizo wachangiaji wengi ni wa economy ujue
 
Mleta mada nisaidie kidogo. Ndani ya Oman air wanatoa huduma za chakula na vinywaji kama Qatar airways au. Sababu napenda Qatar Kwa ajili ya beer za heinken za kopo.
 
Mleta mada nisaidie kidogo. Ndani ya Oman air wanatoa huduma za chakula na vinywaji kama Qatar airways au. Sababu napenda Qatar Kwa ajili ya beer za heinken za kopo.
Ndege tu ndo Ina chata la Oman. Air Ila wahudumu, misosi na huduma zote no Qatar
 
Back
Top Bottom