Qassem Soleiman Alichezea Sharubu za Mmarekani

Qassem Soleiman Alichezea Sharubu za Mmarekani

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,498
Reaction score
28,724
Qassem Soleimani jenerali mkuu wa kikosi cha Quds force huko Iran ameuawa na marekani kwa shambulizi la anga. Huyu ndiye alikuwa anatoa maneno makali sana dhidi ya USA, alimwonya Trump asicheze na Iran, kama sivyo Marekani itajutia kuichokoza Iran. Ila naona sasa yeye ndiye amelazwa chini ya ardhi baada ya kuchokoza maslahi ya Marekani huko Iraq. Trump kasema yeye ndiye katoa ruhusa ya kumuua Qassem Soleimani.

Kiongozi mkuu wa kidini na kitaifa wa Iran Ayatollah Ali Khamanei amesema atalipiza kisasi kwa Marekani dhidi ya shambulio hilo. Kamwonya Trump katika mtandao wa Tweeter kuhusu hilo. Je ni kweli Iran italipiza kisasi kwa Marekani? na kama ndivyo ni nini kitatokea huko mashariki ya kati?

Katika Historia, Nebukadreza mfalme wa Babeli aliishambulia Iran. Elexender mkuu mfalme wa Mecodonia aliishambulia Iran, Roman Empire iliishambulia Iran, Marekani leo naye anataka kuishambulia Iran......????

Iran kihistoria walikuwa ni wababe wa vita, walikuwa ni wataalamu wa kutupa mishale, na walifundishwa kusema ukweli jambo hilo ndilo liliwapa uzalendo katika taifa lao. Siku moja kwa neema ya Mungu nitawazungumzia Irani kwa kirefu.

Karibu kwa maoni.
FB_IMG_1578246171173.jpeg
 
Trump kasema Iran wakilipa kisasi USA watateketeza maeneo 52(52 ni idadi ya raia wa USA waliotekwa na Iran miaka ya nyuma) kwa haraka na nguvu kubwa.

Nawasubiri Iran walipe kisasi.
 
Back
Top Bottom