PVC vs ALUMINIUM Windows

PVC vs ALUMINIUM Windows

ZeMarcopolo

Platinum Member
Joined
May 11, 2008
Posts
14,279
Reaction score
7,681
Wadau,
Nawasalim...

Leo naomba tuongelee madirisha.

New trend in Europe ni utumiaji wa madirisha ya plastic a.k.a plastic windows or PVC windows. Katika nchi hizi madirisha haya yana manufaa zaidi pale yanapowekewa vioo vya layers na kuacha hewa katikati ambayo husaidia kuzuia baridi lisiingie ndani au joto lisitoke nje - isulation.


Madirisha ya plastic kiujumla yana muonekano unaovutia na yako imara sana.

Madirisha ya plastic yanaweza kutengenezwa kwa mitindo mbalimbali ya ufungukaji kama vile kufunguka kwa nje/ndani, ku flip kwa juu au kuslide.


Sijaona nchini Tanzania madirisha haya yakitengenezwa au kuuzwa kwa wingi. Mojawapo wa suppliers wa madirisha haya ni kiwanda kinachomilikiwa na wawekezaji kutoka Uturuki kilichopo Mbezi Beach karibu na SHAMO. (Jina la kiwanda nimelisahau ila lina name PVC na ukipita utaona madirisha haya yamewekwa).

Kama uko kwenye ujenzi na unapenda kuwa na kitu tofauti, jaribu madirisha haya. Hata hivyo ni vyema kutambua kuwa uchache wake unaweza kusababisha bei yake kuwa ya juu kama kawaida ya vitu hadimu.

What is interesting? Utengenezaji wa madirisha ya plastic hautofautiani na ule wa aluminium, lakini for unclear reasons nchini kwetu madirisha ya aluminium peke yake ndio yaliyoshamiri.

Nadhani kwa waliokula chumvi nyingi watakumbuka kuwa madirisha ya aluminium yalipoingia bei yake ilikuwa haikamatiki, lakini siku hizi hata magenge ya kuuza samaki yanatengenezwa kwa madirisha ya aluminium. Hii ni changamoto kwa wawekezaji wa sekta ya ujenzi. Atakayeanzisha kuleta madirisha ya plastic kwa wingi atanufaika sana kabla bei yake haijaporomoka.

Niwatakie siku njema...
 
attachment.php
 

Attachments

  • PVC_windows_and_doors.jpg
    PVC_windows_and_doors.jpg
    88.9 KB · Views: 3,025
Mkuu, haya madirisha yamekuwepo Tanzania for years, maybe over 20 ila yalikua zaidi kwa mahoteli na ofisi, siku za karibuni tumetumia pia kwenye nyumba... wengi wametengeza hata yule jamaa wa kunduchi mzee wa Ngoka pia alikua anatengeneza

the best way for now ni kuyaagiza tu, bado tuna shida ya quality na pia mafundi wetu si waaminifu

nimetumia na kwakweli ni mazuri kuliko ya aluminum
 
Haya madirisha niliyaulizia kuna sehemu moja pale karibu na Victoria, nadhan kwa sasa yapo sehemu nyingi hata hii barabara ya old bagamoyo ohh no sijui yule rais mstaafu wa Kenya kuna sehemu pia wanatengeneza, yana bei hayo. meta moja ya mraba wanauza laki mbili na thelathini.
 
kweli kabisa, ni mazuri na ni fahari kuwa nayo unaonekana wa tofauti,ila ubora wake uko viki kukabiliana na vibaka na wezi kama mwenzangu alivyosema,wanaopindisha nondo,kukata nyavu watayashindwa haya?
 
kweli kabisa, ni mazuri na ni fahari kuwa nayo unaonekana wa tofauti,ila ubora wake uko viki kukabiliana na vibaka na wezi kama mwenzangu alivyosema,wanaopindisha nondo,kukata nyavu watayashindwa haya?
Mkuu kwa swala la wezi na vibaka sidhani hata kwa lile dirisha la aluminium linauwezo wa kufanya ulinzi zaidi ya zile grill zinazotangulizwa ndani na ndio maana kuna nyumba watu wanaishi ndani bila zile aluminium kuwekwa nje wakisubiri wapate haela za kununulia, labda kuhusu ubora ndio unaweza kuzitofautisha alumium na zile za plastic. Nilipouliza kwa moja ya wauzaji kuhusu ubora wa PVC ukilinganisha na Aluminium alinijbu hivi,
PVC nihasa kwajili ya nyumba karibu na bahari...
 
Mkuu kwa swala la wezi na vibaka sidhani hata kwa lile dirisha la aluminium linauwezo wa kufanya ulinzi zaidi ya zile grill zinazotangulizwa ndani na ndio maana kuna nyumba watu wanaishi ndani bila zile aluminium kuwekwa nje wakisubiri wapate haela za kununulia, labda kuhusu ubora ndio unaweza kuzitofautisha alumium na zile za plastic. Nilipouliza kwa moja ya wauzaji kuhusu ubora wa PVC ukilinganisha na Aluminium alinijbu hivi,
PVC nihasa kwajili ya nyumba karibu na bahari...

Mkuu, asante kwa jibu lako.

Huyo aliyekujibu kuwa pVC ni kwa ajili y karibu na bahari alimaanisha kuwa kwa vile PVC hazishiki kutu, lakini sidhani kama hata aluminium inashika kutu.

Mimi zaidi ya uonekano mzuri kingine kinachonivutia kwenye haya madirisha ni jinsi yanavyofunguka. Madirisha ya aluminium mara nyingi huwa naona wanatengeneza sliding style au flipping. Disadvantage ya kuslide ni kwamba dirisha unalitumia nusu tu kwa hiyo kama dirisha lina mita mbili basi unaweza kufungua mita moja tu maximum. Hii sio nzuri kwa upepo na ventilation kwa ujumla. Kuna wakati unahitaji kufungua madirisha yote full nyumba ipate hewa mpya, kwa madirisha ya PVC yanafungua full na unakula upepo full.

Kuhusu vibaka, sidhani kama hata nondo ni solution. Kibaka aliyedhamiria anao uwezo wa kuipúinda au kuikata nodno. Zile grill zina faida ya kisaikolojia zaidi kuliko kuzuia wezi. Madirisha ya aluminium na PVC yote ni ya vioo kwa hiyo mwizi anaweza kuvunja kioo kwa kutumia nyundo au kitu chochote kigumu na kupata access ya nondo ambayo anaweza kuipinda au hata kuikata kwa msumeno tu.
 
Nadhani kuna tofauti kati ya PLASTIC na PVC (Polyvinyl Chloride)........Kuna jamaa wa kituruki hapo opposite na TANESCO mikocheni. Ukweli yanapendeza
 
Vitu vya kifahari ni kwa ajili ya wenye uwezo kifedha. Jambazi anapokwenda kwa mwenye fedha hana shida na madirisha, yeye anapita mlangoni, tena family yote ikiwa nyumbani
 
Nadhani kuna tofauti kati ya PLASTIC na PVC (Polyvinyl Chloride)........Kuna jamaa wa kituruki hapo opposite na TANESCO mikocheni. Ukweli yanapendeza
Na nimependa signature yako...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom