Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,488
- 16,646
Sisi yetu ni macho tu kushuhudia laana inayoendelea kuwapata madhalimu duniani.
Kwa sasa taifa la Marekani chini ya Trump linayumba sana na halijielewi linakoelekea.
Trump amewahi kudai pesa taslim za kile kilichotajwa kuwa ni misaada kwa Ukraine.Aliwahi kufokea mbele ya Kamera na Zelensky halafu akamkaribisha tena ikulu akacheka nae na kumuahidi vitu hewa.
Kiongozi huyo wa taifa kubwa amewahi kuzuia silaha nyeti kuipa Ukraine na baadae ikazitoa bila kuleta mabadiliko yoyote kwa kumegwa kwa ardhi ya Ukraine ambapo Urusi imekuwa ikizidungua moja baada ya nyengine.
Karibuni hivi raisi Trump amekuwa akionesha mahoka ya hali ya juu pale anapotoa makeke kwa Putin wa Urusi baadae kuomba tena urafiki naye.Kichekesho zaidi ni pale alipotoa agizo la mwezi mmoja na nusu kwa Putin afanye makubaliano na Zelensky kumaliza vita.Putin wala hakufanya hivyo.
Siku chache baadae Trump akapeleka nyambizi mbili za nyuklia karibu na Urusi na Putin akampuuza kabisa..Baada ya hapo Trump akapunguza mwezi mmoja na nusu mpaka siku 12.Nazo zimepita bila Putin kutikishika.
Kichekesho kikubwa ni sasa raisi Trump kupanga kukutana na Putin ana kwa ana na kuna tetesi anataka amwachie ardhi za Ukraine ambazo Putin amezinyakuwa kutoa Ukraine.
Trump akubali tu kuwa vita walivyovifadhili vimewashinda na Putin ni mwamba kuliko yeye.