Punguzo la PAYE: Kikwete alitabiri sifa atapata Rais anayemfuatia

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253


Ukifuatilia hiyo clip hapo juu utagundua rais wa awamu nne Mh. Jakaya Kikwete ndiye aliyeshughulikia kwa kiasi kikubwa ishu ya kushushwa kwa kodi ya Pay as You Earn (PAYE).

Alifanikiwa kupunguza kodi kutoka asilimia kumi na nane (18%) hadi asilimia kumi na moja (11%), lengo lilikuwa ni kufikia asilimia tisa.
Alisema mwenyewe kwamba raisi ajaye atajipatia umaarufu kwa kushusha hadi hiyo asilimia tisa.

Hivi kwa kauli hii ya JK, tunaweza kumuita mtabiri?
 
Bavicha wanapokosa cha kuandika huwa ni shiiiidaaaaaa.

Hebu tueleze tatizo nini au ndio jero jero za ufipa ili siku iingie?
 
Kwani kazi ya UKAWA kuwagombanisha JK na JPM??
Ndio wanachofanya sasa hivi.

Jk hana zuri kwao.

JPM hana zuri kwao.

Mapungufu ya Jk wanayasukumizia kwa JPM.

Mazuri ya JPM wanayasukumizia kwa Jk.


Ila wakae wakijua system imeshafunga mkataba na matapeli ya ukawa.
 
Jk awamu ya Nne...unasahau mpaka awamu ya baba yako?Kweli jipu la UDA limeiva,ndio maana Masaburi alimwaga sana hela Ubungo ili ashinde akafiche uchafu wa Machinga Complex na UDA
 
Jk awamu ya Nne...unasahau mpaka awamu ya baba yako?Kweli jipu la UDA limeiva,ndio maana Masaburi alimwaga sana hela Ubungo ili ashinde akafiche uchafu wa Machinga Complex na UDA
Tujadiliane mimi na wewe wazazi wanaingiaje baba yangu umfahamu hata mimi naweza pia kufanya kejeli na matusi kwa wazazi wako kama utapenda nifike huko hamna tatizo tafika lakini usikimbilie kwa Mods.
 
Asanteh sana mkuu kwa uzi huu

Nilichogundu Mh JK alikua na maono sana ya Tanzania ijayo yaani hakutaka sifa zimuangukie yeye bali alimjengea mazingira mazuri Rais ajaye ili asipate shida na hii ndio tunaona kwa Magufuli kila anapogusa ni mterezo tu.

Ki ukweli huyu Rais ataishi mioyoni mwa Watanzania mpaka mwisho wa Dunia huyu ndio aliyetuboreshea mishahara,miundo mbinu,michezo na kuwapa heshima Watanzania wa kuongea na kuhoji hata kama walikuwa wanamtukana.

Kubwa ni kuhakikisha nchi haiingii mikononi mwa watu wabaya na waovu bali alihakikisha anaiacha mikononi salama bila kujari atavunja sheria za chama (mfano;kuingia na majina yake ya mfukoni na kuhakikisha Rais anatoka kwenye majina hayo ingawa wengine hawatakubali) na kumpigania mpaka apate kweli Urais na kafaulu kweli kwa hilo.

Pendekezo: Tumtengenezee sanamu la makumbusho Dar es salaam na Dodoma ili iwe historia kwa vizazi vijavyo.
 
Back
Top Bottom