..nilianzisha uzi nikipendekeza viwanda vya JKT na Magereza vitengeneze barakoa.
Mkuu tumeshauri sana hapa hadi kuambiwa hatuna Uzalendo. Leo kila ulilosema lipo wazi
Nilimwambia
Pascal Mayalla incubation period ikiisha iva kinachofuatia ni community spread katika exponential rate. Ndicho kinatokea. Kesho utasikia wagonjwa zaidi wapya kuliko leo.
Pascal nilisema nitaomba radhi kama haitatokea kwa kupotosha. Uungwana unakuhitaji,nawe sema neno!
Tumepoteza fursa nyingi za kuzuia ugonjwa.Kenya , Uganda na Rwanda walichukua hatua kali mapema, Tanzania ikiwacheka kama anavyoonekana Gwajima n.k.
Tukaruhusu mzaha kama ule wa Makonda ''watoke kuchapa kazi'' . Leo kuna anayetoka?
Wajuvi walifunga maduka, wanajua nini kinaendelea duniani. Hawasubiri kusimuliwa au kushurutishwa.
Tulishauri marufuku ya mikusanyiko hakuna aliyesikiliza. Tukashauri kinga za airborne disease na si kuosha mikono tu na hapa ndipo wangefikiria Barakoa,tulionekana wendawazimu tu.
Hayo yakiendelea akina
MsemajiUkweli walivaa njuga kusifia hata visivyosfikia.
Wakasema Corona inahitaji ''African solution''. Leo hawaonekani tena wamejificha Lumumba baada ya kuupotosha umma. Watakaa kimya vilio vikitanda nchini. Wamepata kula yao kwa gharama za Watanzania.
Hili halina msamaha, corona ilianza China, ikaenda Ulaya na Marekani kabla ya kuja Afrika.
Tulikuwa na kila sababu za kuzuia, viongozi wetu hawakuona hatari au hawakusiklizia walipoambiwa
Na huu ni mwanzo tu, ikifika May 2020 , waliokuwa hawatuelewi watatuelewa.