Punguza kulalamika chukua hatua

Aman Ng'oma

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
954
510
Unapofikiria kufanya ufugaji wa kuku lazima wazo lako likupeleke kwenye kufanya ufugaji wa kuku wa kibiashara ufugaji ambao unakuwa kama kazi. Kwa wanafunzi wanaohitimu vyuo vikuu hawana haja ya kusononeka kwa kuwa hawana kazi lakini badala yake wanaweza wakaitazama fursa ya ufugaji wa kuku kama kazi. Suala litalokuja kuwa changamoto ni mtaji, ndiyo, wahitimu wengi watasema hawana mitaji. Mradi wa ufugaji utafanyikaje bila kuwa na mtaji. Mtaji ni kila kitu .

Mtaji utahitajika katika ujenzi wa mabanda, matunzo ya kuku wenyewe nk. Unaweza kusema huwezi kuanza biashara bila kuwa na mtaji. Lakini sisi tusema hapana, mtaji si kila kitu. Unaweza kuanza biashara bila hata kuwa na mtaji. Mtaji katika kuanza biashara si kitu cha msingi sana. Kitu cha msingi ni wazo. Unapokuwa muhitumu wa chuo kikuu unapaswa kuwa na jicho la kuweza kutazama fursa. Inatakiwa kuamini kuwa mtaani pesa ipo ni wewe tu jinsi utakavyoweza kujipanga. Si wakati wa kulalamika tena. Ni wakati wa kufanya kazi.

Maamuzi yako ndiyo yatakayotengeneza mustakabali wa maisha yako.

Kukosa kwako kazi inatakiwa iwe fursa ya kupima uwezo wako wa kujitegemea baada ya kuhitimu masomo. Wazazi wako wamekwisha kukamilisha wajibu wao kwako. Hutakiwi tena kuendelea kuwa mzigo kwao. Kama ulisoma vyema elimu yako ndiyo silaha ya ukombozi wako.

Ukijaribu kutazama kwa mfano katika mnyororo mzima wa thamani katika ufugaji wa kuku, unaweza kubaini kuwa kuna vifundo vingi ambavyo mjasiriamali anaweza akajishikiza na kuweza kutengeneza pesa. Si lazima wote tulime na wala si lazima wote tufuge. Mazao ya mifugo na kilimo yanajitosheleza sokoni. Na vilevile wakulima na wafugaji waliopo wanatosha kulima na kufuga na kuweza kulisha nchi na ziada ikabaki. Msomi yoyote anapaswa kuwa sehemu ya kusaidia kupatikana kwa ufumbuzi kwa matatizo yanayomkabili mkulima, mfugaji, pamoja na mvuvi.

Hayumkiniki mkulima akahaingika masoko ilihali wasomi wapo. Ni dhambi Mkulima akaendelea kulia na kukosa wa kumfuta machozi yake. Maendeleo ya mkulima ndiyo maendeleo ya Taifa. Tunapaswa kutambua kuwa wakulima ni ndugu zetu, wazazi wetu, kaka zetu na ni dada zetu. Lazima tuwe sehemu ya kutatua matatizo yao kupitia elimu zetu. Nchi yetu ni kubwa na Watazania ni wengi lakini wasomi ni wachache. Tunawajibu kwa watanzania wenzetu. Tuwaongoze ili nao wafurahie kazi ya mikono yao. Lengo ni kuona siku moja kilimo kinatoa sehemu ya matajiri wa nchi hii kama ilivyo katika sekta nyingine za biashara.

Ili kuwasidia wakulima wetu, tunapaswa kwanza kuyajua matatizo yao. Kwa ujumla wakulima wetu wanakabiliwa na maatatizo mengi kwanza kabisa kukosekana kwa tija katika kilimo chao, kwa maana kwamba gharama za uzalishaji zinakuwa kubwa kuliko bei za mazao wanayozalisha. Pili kukosekana kwa mfumo wa uhakika wa masoko. Wafugaji na wakulima wanazalisha mazao lakini wapi wanauza hii inabaki kuwa ni changamoto kubwa kwao. Lakini vilevile kuwepo kwa walanguzi ni kikwazo kikubwa cha kumfanya mkulima aweze kuendelea kwa sababu siku zote mlanguzi huwa kwanza anajitazama yeye binafsi katika biashara na kwa kuwa uwezo wa mkulima wetu kushawishi bei ni mdogo basi anakubali kuuza kwa bei anayopangiwa na mnunuzi kwa kuwa mkulima anakuwa hana namna nyingine hasa ukizingatia kuwa anahitaji pesa kwa ajili ya kugharamia mahitaji yake ya msingi. Kikwazo kingine ni kukokesekana kwa chama madhubuti cha wakulima ambacho kitakuwa sauti kamili ya wakulima kitakachosimama kidete kutetea maslahi yao kama ilivyo kwa wafanyakazi wa uma na sekta binafsi. Vilevile pembejeo za kilimo na mifugo ni ghali mno, ukitazama mboleo bei haishiki, chakula cha kuku halikadhalika. Tija inakuwa ndogo kwa mkulima.

Wakulima na wafugaji wanapaswa kusaidiwa. Nani wa kuwasaidia ni sisi wasomi. Kama tutatimiza wajibu wetu vizuri kwa hakika wakulima wa Tanzania watanufaika na kilimo chao.

Aman Ng'oma
Mkurugenzi wa Kinasoru East Africa (T) Ltd

Mshauri wa Miradi ya Ufugaji wa Kibiashara

0715989713, 0786989713, 0767989713

Dodoma
 
kila mtu kuku.umakin unahitajika isije ikawa high production low demand, watu wakalia na makuku yao.jaribu kuja na idea nyingine jamani
 
maziwa
Mayai
nyama

watanzania bado tuna kiwango cha chini kwa utumiaji wa hivyo vitu... shida vyakula vya mifugo vipo juu ndio maana ukuaji wa uzalishaji haupo sawa na ukuaji wa mahitaji. kuku wa Tanzania ni ghali kuliko aliyetoka Brazil!
tukiweza kudhibiti bei ya chakula kuku in bidhaa bora kibiashara.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom