Mkuu pump zipo za aina nyingi sana, inategemea na size ya shamba lako, binafsi nakushauri hivi; kama shamba lako umeliwekea mabomba and then una connect hose pipes kwa ajili ya irrigation then nunua pump ya 1. 0HP halafu funga automatic system, ukifungua tu bomba lolote na yenyewe inawaka automatic, hiyo automatic inaangalia pressure ilioko kwenye line, haiuzwi bei mbaya kivile, nadhani kwa Dar ni kama Tsh 150k na hiyo sensor ni kama 75k, umeme ndio huo 1.0HP, 2HP=746w, nadhani ipo iko ndani ya uwezo, again haitakua inatembea masaa yote, automatic system itakua inaiwasha pump wakati hitajika tu.