mdukuzi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 20,843
- 51,462

Jana mheshimiwa Rais kapendekeza jina la daraja jipya la kigamboni liitwe daraja la Nyerere Ushauri wa mkubwa ni amri,daraja litaitwa Nyerere Sababu alizotoa ni za msingi sana lakini amini usiamini jina hili litaishia kwenye makablasha tu watu wataendelea kuliita daraja la Kigamboni,hata jiwe la ufunguzi liliandikwa daraja la kigamboni
Zamani Nyerere road ikiitwa Pugu Road kabla ya kubadilishwa jina lakini asilimia kubwa ya watu waliokuwa mjini enzi hizo bado wamezoea kutumia jina la Pugu Road labda wageni ambao hawajui kuwa ile ilikuwa ikiitwa Pugu Road
Natambua mchango mkubwa wa Marais wa Taifa katika nchi hii kuanzia Nyereri Mpaka JPM ila kila kitu kuita majina a viongozi wa kisiasa ni kutaka kudanganya umma kuwa wao ndio wa maana zaidi na kutotambua mashujaa wengine ambao hawakuwa wanasiasa ila wameiletea heshima nchi yetu,kuna watu kama akina Filbert Bayi,Ikangaa,Samatta,na yule mchawi aliyegundua mwenge sijui anaitwa Gonzo sijui nani hao wote ni mashujaa wa nchi yetu,Kuna mitaa maarufu na miundombinu maarufu ingepewa majina yao,sio kila kitu kizuri basi ni Mkapa Tower,Kikwete Hospital,Ali Hassan Mwinyi Road,Mkapa Bridge,Kikwete Bridge,JK Nyerere International Airport.kama Kuendekeza wanasiasa ndio maana barabara inayopita uani mwa ikulu inapewa jina la Barack Obama Drive wakati anayelala humo ni Rais wa Tanzania
kama sio lazima kutumia majina ya watu tutumie majina ya wanyama au vivutio vya utalii au majina ya sehemu husika nikiwa na maana daraja lingeendelea kuitwa kigamboni kama ilivyo mororgoro road,Pugu Road,Kilwa Road hiyo ni njia ya kutangaza utalii