Puerto Rico yapiga kura kujiunga na Marekani

nankumene

JF-Expert Member
Nov 12, 2015
5,916
2,000
upload_2017-6-12_13-23-5.jpeg

Image caption Gavana wa Puerto Rico Ricardo Rossello (katikati) na mkewe Beatriz Rossello (kulia)
Himaya ya Marekani ya Puerto Rico imepiga kura ya kuomba bunge la Congress kuifanya kuwa jimbo la 51 la Marekani.

Zaidi ya asilimia 97 ya wapiga kura walipendelea kujiunga na Marekani badala ya kuwa huru au kuwa himaya tu ya kujisimia.

Hata hivyo asilimia 23 ya wapiga kura walijitokeza kupiga kura licha ya upinzani kususia kura hiyo.

Hata hivyo uamuzi wa mwisho hauko mikononi mwao bali kwa Congress.

Kura hiyo ya maoni ya mwaka 2017 ilitishwa na serikali baada ya kushuhudiwa kwa hali ngumu ya kiuchumi ambayo wengi wanadai kuwa imetokana na hali ya sasa ya Puerto Rico ambayo ni nusu kati ya kuwa na uhuru au himaya linalojisimamia.
upload_2017-6-12_13-22-38.jpeg


Image caption Kulikuwa na maandamano ya kupinga Puerto Rico kwa taifa la 51

Puerto Rico yapiga kura kujiunga na Marekani - BBC Swahili
 

kabwigwa

JF-Expert Member
May 17, 2014
754
1,000
Himaya linalijisimamia au himaya inayojisimamia?himaya upo kwenye ngeli i-zi mfano umoja,himaya imeanguka wingi himaya zimeanguka
 

Ebe

JF-Expert Member
Apr 18, 2013
702
1,000
Ni uboya huu yaan mshindwe kujitegemea mnaomba kuwatwisha wengine mizigo yenu kwa ujinga wenu. Congress wakiwagomea si itakuwa aibu ya karne
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom