Public Service Recruitment Secretariat: Nafasi za kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Public Service Recruitment Secretariat: Nafasi za kazi

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by paesulta, Feb 27, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2012
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  1
  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  OFISI YA RAIS
  SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
  Kumb. Na EA.7/96/01/B/09 22 Februari, 2012
  TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
  Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu
  wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria
  Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na
  kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika
  Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
  Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya
  Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi kwa waajiri mbalimbali katika
  Utumishi wa Umma kama ifuatavyo:
  1.1 AFISA KAZI II ( LABOUR OFFICER II) – NAFASI 3
  Nafasi hizi ni kwa ajili ya Wizara ya Kazi na Ajira
  1.1.1 MAJUKUMU YA KAZI
   Kupokea na kuchambua malalamiko mbalimbali yanayohusu Sheria za kazi
   Kufanya Ukaguzi wa Utekelezaji wa Sheria za Kazi.
   Kukusanya taarifa na takwimu za kazi kutoka sehemu za kazi.
   Kupokea na kuchambua taarifa za migogoro ya kazi.
   Kupokea na kuchambua maombi ya kuandikisha mikataba ya hiari.
   Kupokea na kuchambua madai ya fidia na kiinua mgongo
   Kuandikisha watafuta kazi (job Seekers)
   Kupokea na kuandikisha nafasi za kazi toka kwa waajiri.
   Kupokea nja kuchambua maombi ya vibali vya ajira ya wageni na kutunza
  kumbukumbu za ajira za wageni nchini
   Kukusanya taarifa na takwimu zinazohitajika kwa ajili ya kamusi ya Kazi
  (Dictionary of Occupational Titles )
  2
  1.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   Kuajiriwa wenye Shahada ya Sheria au Uchumi au Sayansi ya Jamii (Sociology) AU
   Stashahada ya juu ya Uendeshaji kazi (Advanced Diploma in Labour Adiministration) kutoka vyuo vinvyotambuliwa na Serikali
  1.1.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi
  1.2 AFISA USHIRIKA DARAJA LA II (COOPERATIVE OFFICER GRADE II) – NAFASI 20
  Nafasi hii ni kwa ajili ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika
  1.2.1 MAJUKUMU YA KAZI
   Kukagua vyama vya Ushirika vya Msingi vinavyoendesha miradi ya pamoja ( Jointy Venture )
   Kuhamasisha uanzishaji wa vyama vya Ushirika vya Msingi.
   Kukusanya na kuchambua takwimu zinazohusu Masoko katika Mkoa.
   Kutoa ushauri juu ya uendeshaji wa Vyama vya Ushirika vya Msingi
   Kuratibu/kushiriki katika Elimu ya Ushirika Shirikishikatika vyama vya ushirika vya Msingi.
  1.2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
  Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya au Stashahada ya Juu (Advanced Diploma) katika mojawapo ya fani za; Ushirika, Uchumi, Uhasibu, au Masoko kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali.
  1.2.3 MSHAHARA
  Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
  1.3 AFISA UGAVI DARAJA LA II (SUPPLIES GRADE II) – NAFASI 1
  Nafasi hii ni kwa ajili ya Wizara ya Mambo ya Ndani
  1.3.1 MAJUKUMU YA KAZI
   Kukusanya takwimu za kusaidia kutayarishwa makisio ya vifaa vinavyohitajika (Material Requirement Budget) na Mpango wa Ununuzi (Procurement Plan).
   Kukusanya na kutunza takwimu za utendaji za Wazabuni mbalimbali.
   Kukusanya na kutunza takwimu za upokeaji, utunzaji, na usambazaji wa vifaa.
   Kusimamia utunzaji wa maghala na hati/kumbukumbu ya vifaa vilivyomo ghalani.
   Kusimamia upokeaji, utunzaji na usambazaji wa vifaa (Physical Distribution).
   Mfumo wa uwekaji na utunzaji wa vifaa ghalani (Location Index Design).
   Kusimamia ukaguzi wa kuhesabu vifaa mara kwa mara (Perpetual Stock Checking) ghalani.
  3
   Kutayarisha Taarifa za kazi katika vipindi maalumu.
   Kuhesabu na kutoa taarifa ya thamani ya vifaa vilivyomo ghalani kila mwisho wa mwaka (Annual Stock Taking).
   Kufanya kazi zingine ambazo atapangiwa.
  1.3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   Kuajiriwa wenye Shahada ya Biashara (B.Comm) yenye mchepuo wa ugavi au Stashahada ya Juu ya Ugavi (Advanced Diploma in Materials Management) inayotolewa na Chuo kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya usimamizi wa Vifaa.
  1.3.3 MSHAHARA
  Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
  1.4 AFISA UGAVI MSAIDIZI (SUPPLIES ASSISTANT) – NAFASI 1
  Nafasi hii ni kwa ajili ya Wizara ya Mambo ya Ndani
  1.4.1 MAJUKUMU YA KAZI
   Kutunza ghala la vifaa lenye thamani ndogo.
   Kupokea vifaa vipya vitakavyoletwa na wazabuni mbalimbli na kupokea vifaa ambavyo vimetumika lakini vinahitaji kutunzwa kabla ya kufutwa.
   Kufungua na kutunza “Bin Card” kwa kila kifaa kilichopo ghalani.
   Kufungua “Ledger” ambayo itatunza kumbukumbu ya vifaa vinavyoingia, kutunzwa na kutoka kwa nyaraka mbalimbali.
   Kutoa vifaa kwa wateja na watumiaji wengine.
   Kuhakikisha kwamba ghala na vifaa vilivyomo vinatunzwa katika hali ya usafi na kwa usalama.
   Kuandaa hati za kupokelea vifaa.
   Kufanya kazi zingine atakazopangiwa.
  1.4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   Kuajiriwa wenye cheti cha “National Store-Keeping Certificate au “Foundation Certificate” kitolewacho na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa au wenye Cheti kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa.
  Au
   Kuajiriwa wenye Diploma ya Kawaida “Ordinary Diploma in Materials Management” kutoka Chuo kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa.
  1.4.3 MSHAHARA
  Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A au TGS B kwa mwezi.
  1.5 KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III – NAFASI 1
  Nafasi hii ni kwa ajili ya Wizara ya Mambo ya Ndani
  4
  1.5.1 MAJUKUMU YA KAZI
   Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
   Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
   Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa wakati unaohitajika.
   Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majadala, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
   Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
   Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
   Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
  1.5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programu za Window, Microstoft Office, Internet, E-mail na Publisher.
  1.5.3 MSHAHARA
  Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi.
  1.6 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU (NYARAKA) DARAJA LA II – (RECORDS MANAGEMENT ASSISTANT GRADE II) – NAFASI 2
  Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam na Kigoma
  1.6.1 MAJUKUMU YA KAZI
   Daraja hili ni la mafunzo katika kazi, hivyo atafanya kazi kwa maelekezo ya Wasaidizi wa Kumbukumbu walio juu yake. Kazi atakazojifunza na kufanya ni zile zifanywazo na Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja I:-
   Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji.
   Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.
   Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
   Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (file racks/cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
   Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk.) katika mafaili.
   Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasisi za Serikali
  1.6.2 SIFA ZA MWOMBAJI
  Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne (IV) au sita (VI) wenye cheti cha utunzaji kumbukumbu katika mojawapo ya fani za Afya, Masjala, Mahakama na Ardhi.
  5
  1.6.3 MSHAHARA
  Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS B kwa mwezi
  1.7 MSAIDIZI WA OFISI (OFFICE ASSISTANT) – NAFASI 2
  Nafasi hizi ni kwa ajili ya Wizara ya Mambo ya Ndani na Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma
  1.7.1 MAJUKUMU YA KAZI
   Kufanya usafi wa ofisi na mazingira ya nje na ndani ikiwa ni pamoja na kufagia, kufuta vumbi, kupiga deki, kukata majani, kupalilia bustani, kumwagilia maji bustani, kupanda maua au miti na kusafisha vyoo.
   Kuchukua na kupeleka majalada na hati nyingine kwa maofsa waoaohusika na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
   Kusambaza barua za Ofisi kama jinsi atakavyoelekezwa.
   Kutayarisha chai ya ofisi.
   Kupeleka mfuko wa posta na kuchukua barua kutoka Posta.
   Kuhakikisha kwamba vifaa vya ofisi vinaweka sehemu zinazostahili.
   Kufungua Milango na Madirisha ya Ofisi wakati wa Asubuhi na Jioni kuyafunga baada ya Saa za Kazi.
   Kudurufu barua au machapisho kwenye mashine za kudurufia.
   Kuweka katika majalada nakala za barua zilizochapwa katika ofisi walizomo.
   Kutunza vifaa vya ofisi na kutoa ripoti kila vinapoharibika.
  1.7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
  Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu vizuri katika masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hisabati.
  1.7.3 MSHAHARA
  Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
  1.8 DEREVA DARAJA LA II (DRIVER II) – NAFASI 5
  Nafasi hizi ni kwa ajili ya ya Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Kazi na Ajira na Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma
  1.8.1 MAJUKUMU YA KAZI
   Kuendesha magari ya abiria, magari madogo na malori
   Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo,
   Kufanya matengenezo madogo madogo katika gari,
   Kutunza na kuandika daftari la safari “Log-book” kwa safari zote.
  6
  1.8.2 SIFA ZA MWOMBAJI
  Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV, Wenye Leseni daraja la “C” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali na wenye Cheti cha Majaribio ya ufundi Daraja la II.
  1.8.3 MSHAHARA
  Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
  NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
  i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
  ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
  iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
  v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzi ngatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka/kupotea.
  - Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
  - Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
  - Cheti cha kuhitimu mafunzo ya kompyuta
  - Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
  - Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
  vii. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  viii. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
  ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Noveba 2010.
  xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  xii. WAAJIRI WOTE WALIOPO NJE YA DAR ES SALAAM WANAOMBWA KUSAMBAZA MATANGAZO HAYA KWENYE MBAO ZA MATANGAZO NA MAENEO MENGINE.
  xiii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 8 Machi, 2012
  7
  xiv. Aidha, matangazo haya yanapatikana kwenye tovoti zifuatazo: PUBLIC SERVICE RECRUITMENT SECRETARIAT - PSRS, Public Service Management na PMORALG - Home -.
  xv. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
  xvi. Kila mwombaji mwenye sifa aonyeshe katika barua yake mkoa anaopenda kufanyia kazi.
  xvii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
  Katibu,
  Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma,
  SLP.63100,
  Dar es Salaam.
  AU
  Secretary,
  Public Service Recruitment Secretariat,
  P.O.Box 63100
  Dar es Salaam.
   
 2. d

  dav22 JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,902
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  safi kabisa...
   
 3. g

  gunasoljer Member

  #3
  Jan 25, 2016
  Joined: Oct 21, 2014
  Messages: 28
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 5
  Hongereni kwa matangazo
   
 4. m

  mundu mkongw Senior Member

  #4
  Jan 25, 2016
  Joined: Jun 10, 2015
  Messages: 185
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Thanx
   
 5. m

  mundu mkongw Senior Member

  #5
  Jan 25, 2016
  Joined: Jun 10, 2015
  Messages: 185
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  kweli watu wana stress tangazo la 2012 umelifufua??
   
 6. vinneboy

  vinneboy JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2016
  Joined: Aug 12, 2015
  Messages: 483
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 80
  yerewiiiiiii
   
 7. Mzee Mchopu

  Mzee Mchopu JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2016
  Joined: Sep 24, 2014
  Messages: 1,037
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Tnx
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...